Mwanamke wa miaka 59 acharazwa viboko baada ya kufumaniwa na kijana kitandani

Muhtasari

•Majirani walimkashifu mwanamke huyo kwa kuwa na tabia ya kuchumbiana na vijana.

Picha ya watu wanaoshiriki katika tedno la ndoa
Picha ya watu wanaoshiriki katika tedno la ndoa
Image: MALAYALAMEMAGAZINE.COM

Mwanamke mmoja amepatana na ghadhabu ya umma kufuatia madai ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kijana.

Kulingana na gazeti la Daily Monitor, mwanamke huyo  kutoka nchi jirani ya Uganda mwenye umri wa miaka 59 anadaiwa kuwa mnyanyasaji sugu  wa kingono.

Majirani walimkashifu mwanamke huyo kwa kuwa na tabia ya kuchumbiana na vijana. Walisema haikuwa sahihi kwake kushiriki tendo la ndoa  na mvulana huyo wa miaka 19.

Walisema kwamba hawangejali ikiwa mwanamke huyo alijihusisha na wanaume wazee badala ya vijana.

"Tulipoingia kwa nyumba ya mshukiwa, tuliwakuta wawili hao kitandani wakiwa uchi na wakaanza kuomba msamaha ... tuliamua kuwapeleka kwenye makao makuu ya parokia ambako tulikuta kijiji kizima kimekusanyika," Jacenta Kamashengyero, mfanyakazi wa kijamii katika eneo hilo alisema.

Gazeti la Daily Monitor liliripoti kwamba viongozi wa eneo hilo hawakutaka kumpiga mwanamke huyo lakini alichagua mwenyewe alipoombwa kuchagua kati ya kazi ya jamii na kupigwa viboko.

“Tulipowakamata wawili hao, tuliangalia adhabu zote; kazi ya jamii na kupiga viboko. Katsigaire alichagua kupigwa viboko na tukaamua kumpa viboko 10 kama onyo kwa wanawake wengine [wenye umri mkubwa],” Bigirwa alisema.

Mwenyekiti wa Kaunti Ndogo ya Kyeizoba, Victor Taremwa pia alitetea adhabu iliyotolewa kwa mwanamke huyo akisema ilikusudiwa kumpa adabu.

Inaripotiwa kwamba mwanamke huyo alitoweka kutoka kijijini hicho baada ya tukio hilo la kutia aibu.