MATOKEO YA KCPE 2021:Orodha ya wanafunzi 10 bora wa KCPE 2021

Muhtasari
  • Magoha alitangaza matokeo hayo mwendo wa saa saba adhuhuri ya Jumatatu katika makao makuu ya Mitihani House Nairobi
Waziri George Magoha katika makao makuu ya KNEC mnamo Machi 28, 2022
Waziri George Magoha katika makao makuu ya KNEC mnamo Machi 28, 2022
Image: ENOS TECHE

Waziri wa elimu George Magoha hatimaye ameachilia matokeo ya mtihani wa KCPE 2021 ambao ulikamilika mapema mwezi huu.

Magoha alitangaza matokeo hayo mwendo wa saa saba adhuhuri ya Jumatatu katika makao makuu ya Mitihani House Nairobi.

Magata Bruce Mackenzie ameibuka mwanafunzi wa kwanza akijizolea alama 428 kati ya alama 500 zinazostahili. Bruce alikuwa mtahiniwa katika shule ya msingi ya Gilgil Hills.

Momanyi Ashley Kerubo kutoka shule ya msingi ya Makini School ameibuka wa pili na alama 427.

 1.Magata Rose Mckenzie -  Gilgil Hills Academy - Alama 428 

2. Momanyi Ashley Kerubo - Makini School - Alama 427 

3. Kwoma Charity Buyanzi -Holy Family Misikhu Girls Primary School- Alama 426 

4. Mbugua Sharon Wairimu - Emmanuel Academy - Alama 426 

5.Muteti Shantel Ndinda - Kitengela International School - Alama 426 

6. Stanley Otieno Omondi - Rofin Field Junior School - Alama426 

 

7. Wekesa Naomi - Whitestar Academy - Alama 426 

8. Kimani Ethan Karuga - Stepping Stones Preparatory -Alama  426 

9. Njeru Joel Junior - Nyagwa Primary -Alama  425

10. Muriuki Victor - PCEA Mwimbi Boarding Primary school-  Alama 425