Ruto amtaka Raila kukoma kutaja jina lake katika kampeni zake

Muhtasari

• Naibu rais William Ruto amemtaka Raila Odinga kukoma kutaja jina lake katika kampeni zake.

• “Koma kutumia jina langu kusukuma kampeni zako, mimi sio manifesto yako,” Ruto alisema.

Aibu rais William Ruto amemtaka kiongozi wa muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga kukoma kutaja jina lake katika kampeni zake na badala yake kuuza sera zake kwa wananchi.

Akiwa katika eneo la Wajir siku ya Alhamisi, Ruto alisema kitendo cha Raila kutaja jina lake kila mara kinaweza kulinganishwa na kukosa ajenda.

“Koma kutumia jina langu kusukuma kampeni zako, mimi sio manifesto yako,” Ruto alisema.

Kinaya ni kwamba Ruto pia amekuwa akimtaja Raila katika kampeni zake akimuita ‘mtu ya kitendawili’ .

Mara si moja naibu rais William Ruto amesikika akimlaumu Odinga kwa kusambaratisha mpago wa ajenda nne kuu za serikali uliolenga kuboresha maisha ya wakenya.

“Msitulaumu wakati ambapo Kenya Kwanza itashinda uchaguzi. Ni kwa sababu hamna ajenda nyingie kado na Ruto,” aibu rais aliogezea.

Naibu rais William Ruto alisema kwamba mrengo wake utashinda uchaguzi kwa asilimia kubwa kwa kuwa wana mpango wa kuwasaidia wakenya.

Aidha, alisema kwamba Raila hapaswi kuzungumzia kuhusu kumaliza ufisadi kwa sababu yeye ni mfaidi mkubwa.

“Atawezaje kupigana na ufisadi wakati yeye ndo amefaidi pakubwa? Pesa anazotumia katika kampeni zake amezipata kiharamu kutoka kwa magavaa,” Ruto aliwaambia wakazi.

 Vilevile Ruto alisema kwamba mswada wa BBI ulikuwa unalenga kuwafaidi viogozi wachache wala sio wakenya.