Familia ya Kibor yazungumza baada ya Raila Kushambuliwa

Muhtasari
  • Familia ya Kibor yazungumza baada ya Raila Kushambuliwa

Familia ya Mzee Jackson Kiprotiich Kibor imejutia kisa cha chopa iliyobeba timu ya kinara wa upinzani Raila Odinga kupigwa mawe eneo la Kabenes huko Uasin Gishu.

Ndege hiyo ilirushiwa mawe huku timu ya Odinga ikiondoka kwenye mazishi ya Kibor siku ya Ijumaa.

Binti ya Kibor Loyce Kiibor anasema majuto yaliyotokea lakini alihusisha na baadhi ya vijana wenye ghasia katika eneo hilo.

Alisema Odinga alifika huku mwili wa Kibor ukiwa tayari umeshushwa kaburini na kukaa nyumbani kwa takriban dakika 20.

“Hatukumtarajia wakati huo kwa sababu mazishi yalikuwa yamekaribia kwisha na hata tulikuwa tumeondoa uwezekano wa kufika kwake”, alisema Loyce.

Alisema pia hawakumtarajia Naibu William Ruto kwa sababu alikuwa ametuma risala zake za rambirambi kwa familia.

Loyce alisema kama familia hawakufahamu kuhusu mpango wowote wa kumshambulia Odinga ambaye alisema alikuwa rafiki wa karibu wa Odinga.

"Tunaomba tu suala hilo lichunguzwe ipasavyo ili mtu yeyote asiye na hatia asilengwe", alisema Loyce.

Alisema babake alipenda amani na mazishi yaliendelea vizuri hadi tukio la dharura lilipotokea.

Mkazi wa eneo hilo Joseph Samoei alisema Odinga alikaribishwa vyema katika eneo hilo lakini matatizo yalianza tu timu ya Odinga ilipoondoka.

Kufikia sasa watu 17 wamo mikononi mwa polisi kuhusiana na shambulizi hilo.