KCSE 2021: Matokeo ya wanafunzi 441 yafutiliwa mbali

Muhtasari

•Waziri wa elimu George Magoha alisema bado wanazuilia matokeo ya shule moja huku uchunguzi wa madai ya wizi ukiendelea. 

Waziri wa Elimu George Magoha katika makao makuu ya KNEC wakati wa kutolewa kwa matokeo ya KCSE 2021 mnamo Aprili,23,2022.
Waziri wa Elimu George Magoha katika makao makuu ya KNEC wakati wa kutolewa kwa matokeo ya KCSE 2021 mnamo Aprili,23,2022.
Image: MERCY MUMO

Matokeo ya watahiniwa 441 wa KCSE 2021 yamefutiliwa mbali kutokana na ripoti za wizi wa mitihani.

Akizungumza wakati wa kutolewa kwa matokeo ya mtihani wa KCSE siku ya Jumamosi, waziri wa elimu George Magoha alisema bado wanazuilia matokeo ya shule moja huku uchunguzi wa madai ya wizi ukiendelea. 

Magoha alisema kesi hizo zilihusisha vifaa visizoidhinishwa katika vituo vya mitihani, simu 203, kesi 223 za uigaji na usababishaji wa fujo.

"Ningependa kusema wazi kuwa KNEC haitakuwa na huruma yoyote kwa wakosaji wa mitihani na lazima wachukuliwe hatua madhubuti," alisema.

Alisema simu nyingi za rununu ambazo zingetumika katika wizi wa  mitihani zilichukuliwa Mwaka jana, wanafunzi 287 waliofanya mtihani wa KCSE wa 2020 hawakupokea matokeo kwa madai ya udanganyifu.

Magoha alisema kuwa kuna ushahidi wa wazi kuwa wanafunzi 287 walihusika katika udanganyifu.

"Kati ya 287, 211 kati yao walikuwa na vifaa visvyoidhinishwa katika vituo vya mitihani… simu za rununu zilikuwa 45," Magoha alisema.