Matokeo ya KCSE kutangazwa leo

Muhtasari

•Matangazo ya matokeo ya KCSE 2021 yanajiri wiki kadhaa tu baada ya watahiniwa kukamilisha mtihani huo.

Waziri wa elimu George Magoha akizungumza siku ya Jumatatu, Aprili 11, 2021
Waziri wa elimu George Magoha akizungumza siku ya Jumatatu, Aprili 11, 2021
Image: MINISTRY OF EDUCATION

Waziri wa Elimu George Magoha anatazamiwa kutoa matokeo ya mtihani wa kitaifa wa KCSE baadae siku ya Jumamosi.

Magoha anatarajiwa kutangaza matokeo wakati wowote kuanzia saa tano asubuhi.

Takriban 831,015 walifanya KCSE katika vituo 10,413 ikilinganishwa na 752,981 ambao walikalia mtihani huo katika vituo 10,437 mwaka 2020. Hili linaonyesha ongezeko la 78,034 au asilimia 9.39.

Kutangazwa kwa matokeo hayo kutafungua njia ya kujiunga na vyuo vikuu, vyuo na taasisi za kiufundi.

Matangazo ya matokeo ya KCSE 2021 yanajiri wiki kadhaa tu baada ya watahiniwa kukamilisha mtihani huo.