Genge la majambazi watano waliojihami kwa panga watiwa mbaroni Mombasa

Muhtasari

•Polisi wameripoti kwamba kila mmoja wa watano hao aalikuwa amejihami kwa panga wakati  walipokamatwa.

Image: TWITTER//NPS

Polisi katika kaunti ya Mombasa wanawazuilia washukiwa watano wa ujambazi wanaoripotiwa kuwa wanachama wa genge maarufu la 'Panga Boys'.

Abdul Charo, Lukman Said Salim,n Mohammed Bwana, Nahim Ongut na Omar Rajab walikamatwa Jumapili asubuhi wakielekea kutekeleza uhalifu katika eneo la Soko Mjinga.

Polisi wameripoti kwamba kila mmoja wa watano hao aalikuwa amejihami kwa panga wakati  walipokamatwa.

Washukiwa pia walipatikana na misokoto ya bangi ambayo itatumika kama ushahidi pamoja na panga tano walizopatikana nazo.

Wakazi ambao wamewahi kuwa wahasiriwa wa genge hilo wameagizwa kufika katika kituo cha polisi cha Mjambere kilicho katika kaunti ndogo ya Kisauni ili kuandikisha ripoti.