Epuka Kufungiwa: Sajili nambari yako ya simu ya Airtel

Bonyeza *106# katika simu yako kuhakikisha usajili wa namba yako ya simu

Muhtasari
  • Bonyeza *106# katika simu yako kuhakikisha usajili wa namba yako ya simu, pamoja na kutazama idadi ya namba za simu zilizosajiliwa kwa namba yako ya kitambulisho.
Airtel Kenya CEO Prasanta Das Sarma.
Airtel Kenya CEO Prasanta Das Sarma.

Wakenya wanahamasishwa kuthibitisha kwamba laini zao za simu zimesajiliwa. Hii ni baada ya tume ya mawasiliano nchini Communications Authority of Kenya (CAK) kutoa agizo hilo. Mkurugenzi mkuu wa CAK nchini, Ezra Chiloba alisema kuwa iwapo unataka kuhakikisha laini ambazo zimesajiliwa na nambari yako ya kitambulisho, unafaa kubonyeza *106# na kisha ufuate maagizo yanayofuata.

Kama wewe ni mteja wa Airtel, fuata maagizo yafuatayo kuhakikisha umejisajili

  1. Bonyeza *106# katika simu yako kuhakikisha usajili wa namba yako ya simu, pamoja na kutazama idadi ya namba za simu zilizosajiliwa kwa namba yako ya kitambulisho.
  2. Kama nambari yako ya simu haijasaliwa unaweza jifanyia mwenyewe kwa tovuti yao https://airtelkenya.com/lp/kyc/ ili kuepuka kufungiwa laini yako.
  3. Unaweza tembelea maduka ya Airtel yaliyo karibu nawe kwa usaidizi zaidi kama unashindwa kusajili laini yako ya simu nyumbani kwenye tovuti yao.
  4. Wateja wote wa Airtel lazima wawe na kitambulisho cha Taifa wakitembelea maduka ya Airtel ili kujisajili.
  5. Airtel inawazawadi wateja watakaosajili nambari zao kwa tovuti yao https://airtelkenya.com/lp/kyc/ ama maduka ya Airtel yaliyo karibu nawe.

Epuka kufungiwa, hakikisha kwamba laini yako ya simu ya Airtel imesajiliwa leo!!!