Hatimaye Hayati Mwai Kibaki azikwa nyumbani kwake Othaya

Muhtasari
  • Tukio la maziko lilikuwa la faragha; iliyohudhuriwa na familia na wageni wachache
Image: EZEKIEL AMINGA

Aliyekuwa Rais wa Kenya marehemu Mwai Kibaki amezikwa nyumbani kwake katika Eneo Bunge la Othaya, Kaunti ya Nyeri.

Tukio la maziko lilikuwa la faragha; iliyohudhuriwa na familia na wageni wachache.

Mwili wa Kibaki ulizikwa karibu na kaburi la mkewe Mama Lucy Kibaki.

Misa ya Mazishi ya Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki ilihudhiriwa na wakenya wa tabaka mbali mbali

Ibada hiyo iliongozwa na Kanisa Katoliki ambalo marehemu alikuwa mshirika.

Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya walihudhuria ibada hiyo