Mkanganyiko baada ya bomu kuonekana Murang'a

Muhtasari

•Inaaminika huenda bomu hiyo iliachwa nyuma miaka ya 1950's wakati wanajeshi wa Uingereza walikuwa wanatumia vilipuzi kuwafurusha Maumau kutoka vichaka vya Mt Kenya na Aberdares.

Bomu lililoonekana Murang'a
Bomu lililoonekana Murang'a
Image: NPS

Bomu linaloaminika kuachwa nyuma miaka mingi iliyopita wakati wa vita kati ya Waingereza na Maumau lilionekana katika kaunti ya Murang'a siku ya Jumapili.

Polisi wameripoti kuwa bomu hilo liligunduliwa katika eneo la Kigumo baada ya familia moja kuripoti kuhusu kifaa tatanishi walichoona nyumbani kwao.

Wataalamu wa bomu katika kaunti ya Murang'a walifika katika eneo la tukio na kudhihirisha kuwa kifaa kili kilikuwa mortar bomb lenye urefu wa milimita 84.

Chombo kile hatari cha vita kilikuwa kimevutia umati mkubwa wa watu, wengi wakitaka kujua watu wengi walitaka kujua kile kitu kinachofanana na nduma  kubwa ni nini hasa.

Wanakijiji waliokuwa wamechanganyikiwa waliwatuma watoto wawili kwa mwanajeshi mstaafu ili awasaidie kutambua kifaa kile. 

Kitengo cha DCI kimeripoti kuwa chifu wa eneo hilo alifikiwa na ripoti hizo na kuwafahamisha polisi kutoka kituo cha Kigumo.

Inaaminika kuwa huenda bomu hiyo iliachwa nyuma miaka ya 1950's wakati wanajeshi wa Uingereza walikuwa wanatumia vilipuzi kuwafurusha wapiganaji wa Maumau kutoka vichaka vya Mlima Kenya na Aberdares.

Ala hiyo ya vita kwa sasa ipo mikononi mwa wataalamu  ambao watasaidia kuiharibu siku ya Jumatatu.