Watu 6 wahofiwa kufariki katika ajali mbaya ya barabarani kwenye barabara ya Mwingi-Thika

Muhtasari
  • Naibu Kamishna wa Kaunti ya Lower Yatta Rebecca Ndiragu alithibitisha ajali hiyo na kifo cha sita hao
  • Ilifanyika kati ya soko la Kanyonyoo na Kivandini
Watu 6 wahofiwa kufariki katika ajali mbaya ya barabarani kwenye barabara ya Mwingi-Thika
Image: KWA HISANI

Takriban watu sita wanahofiwa kufariki kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyohusisha Basi la Garissa na gari la kibinafsi kwenye barabara kuu ya Mwingi-Thika.

Watu sita waliokufa walikuwa kwenye gari la kibinafsi.

Naibu Kamishna wa Kaunti ya Lower Yatta Rebecca Ndiragu alithibitisha ajali hiyo na kifo cha sita hao.

Ilifanyika kati ya soko la Kanyonyoo na Kivandini.

Barabara hiyo inasemekana kujengwa na imekuwa ikihatarisha maisha ya watumiaji wa barabara hiyo.

Ajali nyingine mbaya kama hiyo ilitokea katika Barabara ya Machakos-Kitui Jumamosi usiku na kuua watu kumi na mmoja.

Ajali hiyo ilitokea wakati Matatu walimokuwa wakisafiria iliyokuwa na viti 14 ilipoteza mwelekeo  na kubingiria mara kadhaa eneo la Kanyonyoo huko Kitui.

Naibu Kamishna wa Kaunti ya Lower Yatta Rebecca Ndirangu alisema watu tisa walifariki papo hapo na wengine wawili kuaga dunia kutokana na majeraha walipokuwa wakipokea matibabu katika hospitali ya Kitui Level 5.