Kinoti apongeza polisi kwa kushikilia hisia zao licha ya kejeli za wanasiasa

Muhtasari

• Mkurugenzi wa idara ya uchunguzi wa jinai (DCI) George Kinoti amezungumzia kejeli za hivi majuzi dhidi ya maafisa wa polisi kuhusiana na uwezo wao kimasomo.

• Kinoti alisema ikiwa afisa wa polisi katika eneo ambapo Malala alitoa matamshi hayo angechukuwa hatua kwa hasira basi kusingekuwa na kesi yoyote.

• Kinoti alisema ikiwa afisa wa polisi katika eneo ambapo Malala alitoa mamatamshi hayo angechukuwa hatua kwa hasira basi kusingekuwa na kesi yoyote.

Mkuu wa idara ya DCI George Kinoti
Mkuu wa idara ya DCI George Kinoti

Tunaweza kuwa na changamoto za kimasomo lakini tuna nguvu kihisia, amesema DCI Kinoti.

Mkurugenzi wa idara ya uchunguzi wa jinai (DCI) George Kinoti amezungumzia kejeli za hivi majuzi dhidi ya maafisa wa polisi kuhusiana na uwezo wao kimasomo.

Kinoti alisema ukweli kwamba wengi wao wanaweza kutokuwa na nguvu katika masomo haimaanishi kuwa hawana thamani.

Alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa wananchi milioni 20 kuhusu ujuzi wa kidijitali.

“Badala ya kusherehekea akili zetu za kihisia, unakejeli kisomo chetu," Kinoti alisema.

Alizungumzia maafisa wa polisi waliojihami kwa silaha kali na ambao wanalinda usalama akisema kwamba licha ya kuwa na silaha kali wanadhibiti hisia zao hata wanapodunishwa na kukejeliwa.

"Unapomkasirisha afisa wa polisi anayekutunza ambaye yuko tayari kumwaga damu yake, na amebeba bunduki iliyojaa risasi, huenda akahisi kama raia wa kawaida na kukawa na uwezekano mkubwa wa kujibu," alisema.

Hofu hii imeibuliwa na semi za baadhi ya wanasiasa walionekana kuwakejeli na kuwadunisha maafisa wa polisi.

Mwezi Mei, Seneta wa kaunti ya Kakamega Cleophas Malala akihutubia mkutano wa hadhara alionekana kukejeli kiwango cha elimu cha maafisa wa polisi.

Kinoti alisema ikiwa afisa wa polisi katika eneo ambapo Malala alitoa matamshi hayo angechukuwa hatua kwa hasira basi kusingekuwa na kesi yoyote.

"Huenda asiwajibikie kitendo chake lakini kama afisa wa polisi unahitaji kutupongeza kwa sababu tuna nguvu kudhibiti hisia zetu," aliongeza.