Ruto abadili msimamo kuhusu uagizaji wa nguo za mitumba

Muhtasari

• Ruto alisema hakuna namna makampuni madogo madogo yataangushwa na kikundi kidogo cha wanasiasa wenye maslahi binafsi. 

 

Image: RUTT, TWITTER

Naibu Rais William Ruto amesema utawala wake utalinda na kuunga mkono biashara ya Mitumba nchini. 

Akizungumza siku ya Jumatano katika kaunti ya Mandera Ruto alisema hakuna namna makampuni madogo madogo yataangushwa na kikundi kidogo cha wanasiasa wenye maslahi binafsi. 

"Tutaunga mkono biashara kama hizo kwa sababu zinaendesha uchumi wetu na kuajiri zaidi ya watu milioni mbili," alisema Ruto. 

Alikuwa akizungumza katika miji ya Mandera, Elwak na Tabaka katika Kaunti ya Mandera ambako alifanya mikutano ya hadhara. 

Pia aliongoza Kongamano la Kiuchumi la Kenya Kwanza katika Kaunti ya Mandera. Akilinganisha na mfumo wa uchumi anaopigia debe wa Bottom-Up, Ruto alisema rasilimali zitaelekezwa kwa sekta ya nguo za mitumba.

 "Kwa usaidizi kutoka kwa vijana wenye ujuzi waliofunzwa katika vyuo vya kiufundi, sekta hii itapiga mchipuko wa sekta ya nguo," alieleza. 

Naibu Rais alisikitika kwamba siasa za ulaghai na uongo zilikuwa zimeenea sana nchini kiasi cha baadhi ya wanasiasa kudharau biashara za watu wengine.

 "Mtazamo wa hila unaofahamisha baadhi ya viongozi hawa ndio unaoua uvumbuzi na biashara ndogo ndogo nchini Kenya. Lazima ikataliwe,” alisisitiza. 

Ruto ambaye pia ni Mgombea Urais wa muungano wa Kenya Kwanza, aliwaomba wakazi wa Mandera kuunga mkono serikali itakayojali maslahi yao. 

"Tumekuwa tukifanya mikutano ya kiuchumi ya kaunti kote nchini kwa sababu tunataka kujenga upya uchumi wetu kutoka Chini ambako watu wengi wako.

" Aliongeza kuwa kuna haja ya Wakenya kupiga kura kwa maslahi na matarajio yao. "Pigeni kazi kura kazi.

Piga kura kwa afya bora na elimu kwa watoto wako. Msitumike kama mashine za kupigia kura,” alisema. Mbunge wa wa Garissa Aden Duale alimwomba Naibu Rais kukomesha mauaji ya kiholela Kaskazini mwa Kenya mara tu atakapoingia madarakani. 

"Vijana wetu hawawezi kuendelea kuhusishwa na uhalifu. Ni wakati wa serikali kutoa usalama kwa watu wake na mali zao. 

Kwa siku nne, Dkt Ruto amekuwa katika Mji wa Garissa, Mbalambala na Modogashe katika Kaunti ya Garissa, Habaswein, Hadado, Bute na Kotulo katika Kaunti ya Wajir na Mji wa Mandera, Elwak na Takaba katika Kaunti ya Mandera akipigia debe uungwaji mkono kwa Kenya Kwanza.