Dereva wa Tuktuk apatikana ameuawa Kasarani

Muhtasari

•Mwili wa  Harun Wangendo mwenye umri wa 38, ulipatikana ndani ya tuk-tuk yake kando ya  barabara.

•Polisi wanachunguza kifo cha mtoto mwenye umri wa mwezi saba aliyekufa mkononi mwa mfanyikazi huko Dagoreti,

Crime Scene

Majambazi walitoweka baada ya kutekeleza mauaji ya mwendeshaji tuk-tuk katika mtaa wa Kasarani  jijini Nairobi.

Mwili wa  Harun Wangendo mwenye umri wa 38, ulipatikana ndani ya tuk-tuk yake kando ya  barabara.

Harun aliripotiwa kupotea Jumapili wiki iliopita na mwili wake  kupatikana Jumatatu ndani ya tuk-tuk.

Mkuu wa polisi mtaa wa Kasarani Bw. Peter Mwanzo alisema kuwa huenda Harun aliuawa  kwingineko kisha mwili wake kusafirishwa hadi pale.

‘Hakuna dalili yoyote ya vurugu ulioonekana, ni kama aliuliwa kwingine na mwili kusafirishwa kwa meneo ya tukio kuonyesha kuwa amejiua’alisema

Hakuna yeyote ambaye amekamatwa ilhali uchunguzi bado unaendelea katika juhudi za kuwatambua waalifu walioshiriki katika mauaji hayo, kilicho sababisha kifo chake bado haijajulikana.

Kwingineko polisi wanachunguza kifo cha mwanaume mwenye umri wa 26 ambaye mwili wake ulipatikana nyumbani kwake. Inadaiwa kuwa  huenda alijitia kitanzi katika moja ya vyumba vya wafanyikazi Kabete.

Kisa kama hiki kiliripotiwa Taru, Kwale.

Polisi katika taarifa yao wamesema kuwa kisa hicho cha Kabete kilitokea baada ya marehemu kuzozana na watu ambao hawajulikani. Mwili wake ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi  maiti.

Kesi mingi kama hizi zimekithiri huku polisi sasa wakiwa wanashughulikia 499 zilizofanyika mwaka wa 2019 na 575 mwaka wa 2020.Idadi ya watu 313 wameripotiwa kujitia kitanzi kati ya Januari na Julai mwaka wa 2021.

Polisi wanachunguza  kifo cha mtoto mwenye umri wa mwezi saba aliyekufa mkononi mwa mfanya kazi huko Dagoreti, Nairobi.

Joyness Moraa aliachwa na mamake mkononi mwa mfanyikazi. Baadae alipokea simu akiwa kazini kuarifiwa kwamba mwanawe amefariki.

Mfanyikazi aliambia polisi kuwa alilisha mtoto na kumuacha apumzike malazini,aliporudi alipata mtoto ametulia na hasongi ndiposa akajuuza mamake.

Mwili ulipelekwa kwa makafani ilikufanyiwa uchunguzi zaidi ili kubaini ni nini kilicho sababisha kifo cha mtoto huyo mchanga.