DCI yafichua genge la 'Confirm Gang' lililosababisha mauaji Nakuru

Muhtasari
  • Wahudumu wa DCI wamefichua nyuso za wanachama wa genge maarufu kwa jina la 'conirm gang'.
DCI wamefichua nyuso za wanachama wa genge maarufu kwa jina la 'conirm gang'.
Image: DCI/TWITTER

Wapelelezi wa DCI wamefichua nyuso za wanachama wa genge maarufu kwa jina la 'conirm gang'.

Kulingana na DCI, maafisa wa upelelezi walimtia mbaroni mpangaji mkuu wa mauaji ya Nakuru Kaskazini.

Evans Kebwaro alikamatwa na washirika wengine watano huko Keroka, kaunti ya Kisii. Julius Otieno, Josephat Simiyu, Dennis Nmblo na Isaac Kinyanjui wanaaminika kuhusika na mauaji ya hivi majuzi ya Mawanga.

"Maafisa wa upelelezi wamekamilisha uchunguzi unaohitajika wa mahakama na kuweka nyaraka za wanachama 6 wa genge, waliohusika na mauaji ya kiholela yaliyorekodiwa huko Nakuru Kaskazini, katika siku za hivi majuzi. Hii inafuatia operesheni ya kina iliyofanywa na wapelelezi."Ilisoma taaria ya DCI.

Siku chache zilizopita, wanawake watano waliuawa na miili yao kuchomwa Nakuru.

Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i amewahakikishia wakazi wa Nakuru kwamba wahalifu hao watakamatwa katika muda mfupi iwezekanavyo. Amri ya kutotoka nje pia iliondolewa kama njia ya kuwasaka wahalifu.

Watafikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya mauaji iwapo watapatikana na hatia.

"mshtuko wa maisha yao bado. Vumbi likitimka kufuatia zogo la kuwasili na kukosa pa kukimbilia, watano hao walijisalimisha mikononi mwa mawakala wetu, kwani walikuwa wageni wa mwisho wa serikali.

Sita hao kwa sasa wanashughulikiwa ili kujibu mashtaka ya uhalifu wao."