•Katibu Mkuu Wizara ya Afya Susan Mochache ambaye alikuwa ni mgeni mkuu wakati wa uzinduzi huo
•Gavana wa Kaunti ya Meru Kiraitu Murungi ambaye pia alihudhuria hafla hiyo alisema kuwa Mahakama inafaa kuwa makini na kutoa adhabu kali kwa wahusika
Kaunti ya Meru imeorodheshwa katika nambari ya tatu kwa visa vya ukatili wa kijinsia na mimba za mapema miongoni mwa Vijana, hii ni kulingana na afisa mkuu wa Afya ya umma John Inanga.
Haya iliwekwa wazi na mkuu huyo wakati alikuwa akizungumza katika chuo cha Mafunzo ya ualimu Meru katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia na mimba za mapema dhidi ya vijana katika Kaunti hiyo.
''Ukatili wa Kijinsia, maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na mimba za mapema ni shida kubwa sana hapa, ni jambo ya kushangaza'' Inanga alisema.
Pia aliongeza kuwa wanafanya kila juhudi zinazopaswa kuchukuliwa ili kupunguza viwango vya juu vya maambukizi ya Virusi vya Ukumwi, na Ukatili wa Kijinsia.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Susan Mochache ambaye alikuwa ni mgeni mkuu wakati wa uzinduzi huo aliwarai Viongozi wa Siasa na washikadau wa Serikali kukuwa mstari wa mbele kuhamashisha umma kuhusu jinsi ya kuepukana na changamoto hizo.
''Visa vya maambukizi ya Ukimwi vimeongezeka, watu wengi wamesahau kuchukua tahadhari juu ya maambukizi hiyo ,badala yake wanazingatia namna ya kujikinga dhidi Janga la Korona kuliko ugonjwa wa Ukimwi'' Mochache alisema.
Gavana wa Kaunti ya Meru Kiraitu Murungi ambaye pia alihudhuria hafla hiyo alisema kuwa Mahakama inafaa kuwa makini na kutoa adhabu kali kwa wahusika wanaoeneza Ukatili wa Kijinsia badala ya kuwawacha kwa dhamana.
''Mimba za mapema miongoni mwa Vijana ni kwasababu ya Ukatili wa Kijinsia ambapo pia huchangia pakubwa kwa usambazi wa Ugonjwa wa Ukimwi miongoni mwa Vijana,'' Kiraitu alisema.