Jamaa taabani baada ya kupatikana na simu 93 Nairobi

Mshukiwa alitiwa mbaroni baada ya kushindwa kuthbitisha umiliki wa simu hizo.

Muhtasari

•Brian  Mutua Muema alikamatwa na maafisa kutoka kituo cha Kware, Embakasi baada ya kupatikana na simu 93. 

•Mshukiwa alitiwa mbaroni baada ya kushindwa kutoa maelezo kamili ya kuthibitisha umiliki wa simu hizo.

Mshukiwa Brian Muema
Image: NPS

Maafisa wa polisi katika kaunti ya Nairobi wanamzuilia jamaa mmoja kwa madai ya wizi wa simu za mkono.

Brian  Mutua Muema alikamatwa Ijumaa na maafisa kutoka kituo cha Kware, Embakasi baada ya kupatikana na simu 93. 

Polisi waliofika kwenye makazi ya mshukiwa katika eneo la Pipeline walipata aina mbalimbali za simu za rununu zinazoshukiwa kuibiwa.

Tume ya Huduma kwa polisi polisi walikuwa wamepokea taarifa za kijasusi kutoka kwa umma wakati walitembelea chumba hicho cha kukodi na kupata simu hizo.

Mshukiwa alijiipata taabani baada ya kushindwa kutoa maelezo kamili ya kuthibitisha umiliki wa simu hizo.

Mara moja maafisa hao walishuku kuwa simu hizo zilikuwa zimebiwa na kumtia pingu mshukiwa. 

Muema kwa sasa yuko rumande akisubiri kufikishwa mahakamani Jumatatu huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

NPS iliwataka wananchi kujitolea kutoa taarifa  kuhusu watu wanaowatilia shaka au shughuli zao, na kuongeza kuwa utoaji taarifa ni chombo chenye ufanisi zaidi katika vita dhidi ya uhalifu.