Bei ya gesi yashuka baada ya serikali kupunguza kodi

Bei imeshuka kwa kati ya Sh100 na Sh250 baada ya VAT kupunguzwa kutoka 16% hadi 8%.

Muhtasari

•Bei ya gesi ya kupikia imeshuka kwa kati ya Sh100 na Sh250 kufuatia kupunguzwa kwa Kodi ya VAT  kutoka asilimia 16 hadi asilimia 8.

•Kupunguzwa kwa bei hiyo kunafuatia kupitishwa kwa Sheria ya Fedha, 2022, iliyorejelea VAT kwenye Gesi ya Petroli ya Kimiminika (LPG).

Mitungi ya gesi
Mitungi ya gesi
Image: MAKTABA

Bei ya gesi ya kupikia imeshuka kwa kati ya Sh100 na Sh250 kufuatia kupunguzwa kwa Kodi ya VAT  kutoka asilimia 16 hadi asilimia 8.

Ukaguzi wa VAT ulifanyika wiki mbili zilizopita lakini Jumatatu ndio siku ambayo bei mpya za rejareja zilitangazwa.

Kupunguzwa kwa bei hiyo kunafuatia kupitishwa kwa Sheria ya Fedha, 2022, iliyorejelea VAT kwenye Gesi ya Petroli ya Kimiminika (LPG).

Wafanyibiashara wamepunguza bei ya kujaza mtungi wa  kilo sita na kati kwa Sh100-150 na wa kilo 13 kwa Sh200-250.

Mwongozo mpya wa orodha ya bei katika duka la Shell huko Westlands unaoshikamana na Afrigas unaonyesha kuwa kujaza tena silinda ya kilo 6 sasa ni Sh1,440 kutoka Sh1,560 na 13kg sasa ni Sh3,100 kutoka Sh3,350.

Maduka ya Shirika la Taifa la Mafuta la Kenya jijini Nairobi yanajaza tena mtungi wa kilo 6 wa Supa Gas kwa Sh1,400 kutoka Sh1,500 na mtungi wa kilo 13 kwa Sh3,050 kutoka Sh3250.

David Muo, mchuuzi wa Juja, kwa sasa anajaza tena silinda ya kilo 6 kwa Sh1,300 kutoka Sh1,450 na kilo 13 kwa Sh2,800 kutokaSh3,050.

Muo alisema kuwa awali bei ya jumla ya mitungi yote isipokuwa ya kimataifa na Pro Gas ilikuwa Sh190 kwa kilo.

Pro Gas ilikuwa Sh202 kwa kilo na ya kimataifa (K-gesi, Jumla, OiLibya, Afri, n.k) ilikuwa 200 kwa kilo.

"Kwa sasa tunapata Pro Gas kwa Sh188 kwa kilo, kimataifa kwa Sh185 kwa kilo na mitungi mingine Sh178 kwa kilo," alisema Muo.

Hii ni tafsiri ya bei ya jumla ya Sh1,128 kwa mtungi wa kilo 6 kutoka Sh1,212 na Sh2,444 kwa kilo 13 kutoka Sh2,626 kwa Pro Gas ambayo ni ghali zaidi ya mitungi yote.

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli haidhibiti bei ya gesi ya kupikia.

Hii inamaanisha kuwa bei yake inaamuliwa na nguvu za soko za mahitaji na usambazaji, jambo ambalo huwapa wafanyabiashara uhuru wa kupanga bei ya bidhaa zao kulingana na mienendo ya soko.

Jana, bei ya mafuta ghafi duniani ilishuka kwa pointi 12 hadi chini ya $95 kwa pipa kwa mara ya kwanza tangu Urusi kuivamia Ukraine.

Brent, alama ya kimataifa, ilishuka hadi $94.50 kwa pipa. Ilifungwa kwa $96.84 mnamo Februari 23, siku moja kabla ya Urusi kuivamia Ukraine.

Hili linatarajiwa kushuka zaidi wakati Shirika la Nchi Zinazouza Nje ya Petroli (OPEC) likikutana Alhamisi hii.

Lengo kuu la mkutano huo litakuwa kujadili mikakati na mipango ya kuongeza uchimbaji wa mafuta katika nchi nyingi.

Huku bei ya mafuta ghafi ikishuka katika siku mbili zilizopita, kuna nafasi nzuri kwamba makampuni ya uuzaji wa mafuta yatazingatia kupunguza bei ya LPG.

Gesi ya kupikia kwa sasa inaagizwa na wafanyibiashara wa kibinafsi na inawapa uwezo wa kupanga bei yao, lakini kituo cha watumiaji wa kawaida kitawezesha LPG kuagizwa kutoka nje kupitia mfumo wa zabuni huria (OTS) ambapo makampuni yatashindana kuagiza LPG ya bei nafuu zaidi. 

Ola Energy imepanga kupanua uwezo wake wa kuagiza na kuhifadhi LPG hadi tani 15,450 kutoka tani 450 kufikia mwaka ujao huku ikitafuta sehemu kubwa ya soko la gesi ya kupikia.

 Kampuni ya Kenya Pipeline (KPC) pia inatazamiwa kujenga kituo cha kuhifadhi LPG katika Kenya Petroleum Refineries Ltd (KPRL) katika hatua ya kurahisisha uagizaji wa gesi ya kupikia nchini. 

Wauzaji wa mafuta sasa wanaangalia ongezeko la mahitaji ya bidhaa hiyo kote nchini Kenya na kanda kubwa ya Afrika Mashariki. 

Takwimu kutoka Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya zinaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko la mahitaji ya LPG nchini Kenya huku matumizi yakifikia tani 182,540 mnamo Desemba 2021, kutoka tani 167,200 mwaka uliopita.