Kenya yapokea mkopo wa shilingi bilioni 27.8 kutoka IMF

Muhtasari

• Kiasi hicho kitatumika kupiga jeki bajeti, na kufikisha jumla ya malipo ya Kenya kwa usaidizi wa bajeti hadi sasa kufikia takriban $1.208 bilioni.

Image: HISANI

Kenya imepokea mkopo wa dola mlioni 235.6 (Sh. B.27.8) kama sehemu ya hazina ya kukinga nchi iliyoidhinishwa Aprili mwaka jana.

Hii inafuatia kukamilika kwa ukaguzi wa tatu chini ya mpango wa miezi 38 na chini ya Mpango wa nyongeza ya Mikopo (ECF) na Mpango wa Hazina Iliyoongezwa (EFF) na bodi ya IMF mwishoni wa siku ya Jumatatu.

Pesa hizo zitatumika kupiga jeki bajeti, na kufikisha jumla ya takriban dola bilioni 1.208 pesa ambazo Kenya imetenga kusitiri bajeti kufikia sasa.

Hii ni sehemu ya mkopo wa dola bilioni 2.34 ulioidhinishwa na shirika la fedha duniani kwa Kenya mnamo Aprili 2, 2021.

Ingawa umecheleweshwa sana, mkopo huo unatarajiwa kuimarisha akiba ya fedha za kigeni nchini Kenya ambayo imekuwa ikipungua huku Benki Kuu (CBK) ikisambaza dola zaidi sokoni kusaidia kustawisha shilingi ambayo tangu wakati huo imeshuka hadi 118 dhidi ya dola.

IMF ilisema mkopo huo unaleta ustahimilivu kwa kusaidia nchi kukabiliana na majanga ya kimataifa wakati bado inaafikia malengo ya mamlaka na kuendelea kupiga hatua katika kushughulikia udhaifu wa deni.