Viongozi wa Kenya Kwanza watilia shaka uchaguzi wa Agosti 9

Wanataka rais Uhuru Kenyatta kutojihushisha na uchaguzi mkuu unaokuja wiki tatu kutoka sasa.

Muhtasari

• Wanasiasa hao pia walidai kuwa hakuna usalama wa kutosha kwa maafisa wa Tume ya  uchanguzi na mipaka (IEBC).

• Wanataka Tume ya Uchaguzi na mipaka (IEBC) kuwahakikishia kwamba uchanguzi wa Agosti 9 utakuwa wa haki na huru.

Kinara wa ANC Musalia Mudavadi
Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi Kinara wa ANC Musalia Mudavadi
Image: Musalia mudavadi/TWITTER

Viongozi wa Kenya kwanza sasa wanataka Tume ya Uchaguzi na mipaka (IEBC) kuwahakikishia kwamba uchanguzi wa Agosti 9 utakuwa wa haki na huru.

Wakizungumza na wanahabari, viongozi hao walisema kuwa rais Uhuru Kenyatta ameenda kinyume na sheria za humu nchini kwa kujihushisha katika siasa.

''Nataka kumuuliza rais jinsi gani wewe na serikali yako ni mwaminifu kwa katiba ya Kenya, haswa kwa uchaguzi wetu wa kidemokrasia, uchaguzi huru na wa haki, je wewe ni mwaminifu kiasi gani'' Mudavadi aliuliza.

Wanasiasa hao pia walidai kuwa hakuna usalama wa kutosha kwa maafisa wa Tume ya  uchanguzi na mipaka (IEBC).

''Kuna mpango wa udanganyifu ya uchaguzi mkuu na wapinzani wetu, na tunafahamu ushirikiano walionao na wale wageni wa kigeni kuhusu uchaguzi, lakini hatutawaruhusu,'' Duale alisema.

Timu hiyo pia  iliwarai Wakenya kujitokeza na kupiga kura Agosti 9 bila wasiwasi wowote kwani wanaamini kuwa Naibu wa Rais William Ruto atashinda uchaguzi huo.

''Tutakuwa macho kuona jinsi uchaguzi utakavyoendeshwa ili kuepusha udanganyifu wa aina yoyote, Wakenya lazima wafahamiswe  kuhusu shughuli zote ya uchaguzi,'' Duale  alisema

Haya yalijiri baada ya Viongozi kutoka mirengo ya Kenya Kwanza kudai kuwa wanafahamu pia uwezokano wa Wapinzani wao kukuwa na kituo mbadala ya kujumuisha kura

''Tume ya uchaguzi na mipaka wanafaa kuhakikisha kuwa vifaa vya uchaguzi kufika maeneo tofauti kwa wakati unaofaa,''  Duale alisema

Pia walidai kuwa kukamatwa kwa raia wa Kigeni na baadhi vya stika ya IEBC ni mojawapo ya njia ambayo serikali inataka kutumia kuhakikisha kuwa uchaguzi isikuwe wa haki na huru

''Kama walikuwa na hatia ya kupatikana na hizo stakabadhi basi kisheria hawangewachwa,wangefikishwa mpaka mahakamani,lakini waliachiliwa badaye'' Wetangula alisema.