Wazazi wafurahia kuhamishwa kwa shule ya msingi ya Mbiici kutoka maeneo ya uuzaji pombe

hali ya Shule hiyo kuwa kwa eneo la uuzwaji mvinyo kumezorotesha zaidi shughuli za elimu

Muhtasari

• Unywaji mwingi wa pombe na baadhi ya matukio ya kushangaza  karibu na shule hiyo umezorotesha shughuli za masomo

Mbunge Wanjiku Kibe
Mbunge Wanjiku Kibe
Image: HANDOUT

Wazazi wa Shule ya Msingi ya Mbichi walisherekea mpango wa kuhamisha shule iliyo katika kituo cha biashara kilichoathiriwa na pombe.

Wazazi ambao watoto wao wanasoma katika Shule ya Msingi ya Mbichi huko Gatundu Kaskazini wameeleza furaha yao  baada ya Mbunge wa eneo hilo Wanjiku Kibe kununua ardhi mpya ili kuhamisha shule hiyo ambayo kwa sasa iko katika kituo cha biashara hiyo ya pombe.

Kulingana na wazazi, eneo la shule yao limezidi kuzorotesha ufaulu wa watoto wao kwani wanashindwa kuwa makini wakati wa mafunzo kutokana na kelele  za magari, pikipiki na malori yanayoendeshwa kando ya uwanja wa michezo wa shule hiyo.

Wakizungumza wakati wa makabidhiano ya ardhi mpya ambapo Kibe, kupitia NG-CDF wanapanga kujenga shule hiyo kwenye ardhi mpya.

Wazazi walieleza furaha  yao na kusema  kwamba hata watoto waliopelekwa katika shule za kibinafsi kutokana na matatizo yaliyotajwa hapo juu wataanza tena kusoma katika shule zao za umma.

Alisema kuwa baada ya kukamilika kwa kazi za ujenzi, NG-CDF itanunua ardhi ingine  ili kuipa shule eneo la kutosha kuendesha shughuli zao kwa urahisi.

Kibe analenga kutetea kiti chake  tena dhidi ya wagombeaji 16 wa kiume. Alisema atajishughulika katika kubadilisha mazingira ya shule za upili katika muhula wake wa pili.