John Ngumi amridhi Michael Joseph kama mwenyekiti wa Safaricom

Kampuni hiyo pia ilitangaza kujiuzulu kwa Katibu Mdlalose Sitholizwe.

Muhtasari

•John Ngumi ataanza kazi kirasmi mnamo Agosti 1, 2022 huku akichukua nafasi ya Michael Joseph.

Mwenyekiti John Ngumi
Image: ENOS TECHE

John Ngumi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Bodi mpya wa kampuni ya huduma za simu ya Safaricom PLC.

Ataanza kazi kirasmi mnamo Agosti 1, 2022 huku akichukua nafasi ya Michael Joseph.

Kampuni hiyo pia ilitangaza kujiuzulu kwa Katibu Mdlalose Sitholizwe.

Ngumi ni mmoja wa wafanyikazi wa benki maarufu nchini Kenya.

Katika kipindi cha miaka 35 cha kazi yake, alijiimarisha kama mwanabenki mkuu wa makampuni na uwekezaji katika Afrika Mashariki akifanya kazi na makampuni ya nchini na kimataifa ambayo yana uwepo wa kanda ya Afrika Mashariki.

Yeye ni mkurugenzi mwenye uzoefu amkubwa aliojizolea katika kampuni za kibinafsi na biashara zinazomilikiwa na serikali.

Kwa upande wa pili, anajulikana zaidi kama mwenyekiti wa bodi ya uzinduzi katika Mamlaka ya Maendeleo ya Konza Technopolis na amekuwa mwenyekiti wa bodi mwenye bidii katika kampuni ya Kenya Pipeline Limited.

Kwa sasa Ngumi anahudumu kama Mwenyekiti wa Bodi katika Shirika la Maendeleo ya Viwanda na Biashara ambalo linaongoza juhudi za kutekeleza Mtandao wa Usafirishaji wa Kenya unaojumuisha Mamlaka ya Bandari ya Kenya, Kampuni ya Kenya pipeline Limited na Shirika la Reli la Kenya.