Dereva wa mbunge wa Lungalunga Khatib Mwashetani Miongoni mwa 4 waliofariki katika ajali ya barabarani

Wanne hao waliripotiwa kufanya kampeni za kuchaguliwa tena kwa Mwashetani wakati kisa hicho kilipotokea.

Muhtasari
  • Dereva wa mbunge wa Lungalunga Khatib Mwashetani Miongoni mwa 4 waliofariki katika ajali ya barabarani
Image: KWA HISANI

Watu wanne, miongoni mwao wakiwa dereva wa Mbunge wa Lungalunga Khatib Mwashetani, Alhamisi walipoteza maisha katika ajali ya barabarani eneo la Lungalunga kaunti ya Kwale.

Ripoti za polisi zinasema kuwa tairi moja ya gari ambalo wanne hao walikuwa wakisafiria wakati huo, lilipasuka kabla ya gari hilo kubingiria mara kadhaa.

Wanne hao waliripotiwa kufanya kampeni za kuchaguliwa tena kwa Mwashetani wakati kisa hicho kilipotokea.

Kulingana na OCPD wa Lunga-Lunga Peter Mutua Zimbi, wanne hao walikuwa wakielekea Lunga-Lunga kutoka Msambweni.

"Inaaminika kuwa walikuwa wakitoka kwenye mkutano wa kampeni na walikuwa wanakimbia kurejea Lunga-Lunga," alisema.

OCPD alisema ni Toyota Prado.

Uchunguzi wa awali wa polisi ulibaini kuwa dereva huyo alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi.

Gari hilo lilibingiria mara kadhaa, takriban mita 50 kutoka barabarani.

Gari walilokuwa wakisafiria lilikuwa limebeba watu watano.

Miili ya wanne hao imehamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha eneo hilo ikisubiri uchunguzi wa maiti huku mabaki ya gari hilo yakivutwa hadi kituo cha polisi eneo hilo.

Mbunge wa LungaLunga ampoteza dereva wake katika ajali ya barabara