Nyumba ya DPP Noordin Haji Nairobi Yavamiwa na Majambazi

DPP Haji hakuwepo nyumbani wakati wa uvamizi huo.

Muhtasari

•Polisi walifika eneo la tukio na kunakili chini vifaa vilivyoibiwa huku  wakisubiri kuanza  uchunguzi.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji
DPP Norrdin Haji Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji
Image: Maktaba

Makao ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji katika kitongoji cha Riverside jijini Nairobi yalivunjwa usiku wa Alhamisi, Agosti 5, na watu wasiojulikana.

Kulingana na ripoti ya polisi, idadi isiyojulikana ya majambazi walivamia makazi ya DPP na kuiba vifaa vya elektroniki.

Moja wa vyombo vya habari humu nchini iliripoti kuwa wakati wa uvamizi huo, mfanyakazi wa nyumba wawili na watoto walikuwa ndani ya nyumba hiyo lakini hakuna aliyesikia chochote.

DPP Haji hakuwepo nyumbani wakati wa uvamizi huo.

Majambazi hao walitoweka na tarakilishi mbili, TV ya Samsung ya inchi 75, Sony PlayStation 4, viatu vya aina mbalimbali na mifuko miwili.

Polisi walifika eneo la tukio na kunakili chini vifaa vilivyoibiwa huku  wakisubiri kuanza  uchunguzi.

Huduma ya Polisi ya Kitaifa tangu wakati huo imeimarisha ulinzi katika makazi hayo hata kama wanawasaka majambazi.

Kufuatia wizi huo, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (ODPP) ilithibitisha kutokea kwa wizi huo. Hata hivyo, ilitupilia mbali taarifa kwamba ofisi hiyo pia ilivamiwa na majambazi hao.

“DPP angependa kufafanua kuwa kulikuwa na wizi kwenye makazi yake, si ofisi yake, na uchunguzi unaendelea.ODPP, kama Mamlaka ya Mashtaka, haisanyi au kuhifadhi ushahidi wa aina yoyote. Umma na vyombo vya habari wanahimizwa kutoingiza siasa kwenye tukio hili,"  Baadhi ya maneno kutoka taarifa hiyo ilesema.

Ijapokuwa usalama umeimarishwa katika maeneo mbalimbali nchini, idadi ya majambazi wanaovamia nyumba katika mashamba ya kifahari jijini Nairobi pia imeongezeka.