Msiwe na shaka, Ruto atashinda kesi- Gachagua

Rigathi amewataka Wakenya kutoruhusu rufaa iliyowasisilishwa mahakamani na Raila kutamba akilini mwao.

Muhtasari

•Rigathi Gachagua, amewashukuru wakazi wa kaunti ya Nakuru kwa kujitokeza kupigia chama cha UDA kura.

•Amewataka Wakenya kutoruhusu kesi ya mahakama kutamba akilini mwao akidai kuwa ana imani Ruto ataibuka mshindi 

Naibu wa rais mteule,Rigathi Gachagua akihutubu katika eneo bunge la Rongai, Kaunti ya Nakuru.
Naibu wa rais mteule,Rigathi Gachagua akihutubu katika eneo bunge la Rongai, Kaunti ya Nakuru.
Image: HISANI

Naibu wa rais mteule katika muungano wa Kenya Kwanza, Rigathi Gachagua, amewashukuru wakazi wa kaunti ya Nakuru kwa kujitokeza kupigia chama cha UDA kura.

Akizingumza katika eneo bunge la Rongai, alikozuru kumpigia kampeni mgombea kiti cha ubunge kwa tiketi ya United Democratic Alliance (UDA), Chebor, Gachagua amewahakikishia wananchi kwamba serikali ya Kenya Kwanza itatekeleza majukumu yake.

"Nyinyi mlimaliza kazi yenu. Sasa tuachie mimi na Ruto tufanye kazi maana sisi sio walevi na wala hatulei watoto. Tuko na muda wote kuwahudumia wakenya,"Alisema Gachagua.

Ikiwa ngome ya Kenya Kwanza, UDA ilijizolea kura katika nyadhifa mbalimbali kwanzia kiti cha Useneta,Ugavana, madiwani na hata wabunge katika kura kuu za Uchaguzi zilizo kamilika wiki mbili zilizopita.

Aidha, amewahakikishia wananchi usalama na amewaomba kujihusisha na shughuli za kutafuta riziki kama njia moja ya kujiendeleza.

Kadhalika amewataka Wakenya kutoruhusu rufaa iliyowasilishwa mahakamani na Raila kutamba akilini mwao akidai kuwa ana imani Ruto ataibuka mshindi September 5.

"Nawaomba mdumishe amani. Fanyeni kazi. Kesi katika mahakama ya upeo itapita na Ruto kuibuka mshindi," Alisema.

Gachagua aliambatana na wanasiasa wengine wa Kenya Kwanza wakiwemo Kipchumba Murkomen(Elgeiyo Marakwet), Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro na wengine