JAZIKA NA SHELL LUBRICANTS

Ng’amua Habari Bandia

Kununua lubricants ghushi hakuathiri tu ufanyikazi mzuri wa injini yako, bali pia inakugharimu pesa kwa muda mrefu.

Muhtasari
  • Wateja watapiga *459* 200# na kuweka kodi iliyo chini ya kifuniko cha mafuta ili kujiandikisha na kushiriki.
  • Kununua lubricants ghushi hakuathiri tu ufanyikazi mzuri wa injini yako, bali pia inakugharimu pesa kwa muda mrefu.

Huenda sote tumewahi kuanguka kwenye mtego wa habari za uwongo na mara kwa mara tumeambiwa tuthibitishe ikiwa mambo tunayosoma mtandaoni ni ya kweli au ya uwongo.

Wakati mwingine si rahisi kubaini ni nini ghushi na ndiyo maana tunapaswa kuthibitisha habari tunazokutana nazo mtandaoni kama ni za kweli au za uwongo. Kulingana na Shirika la Kupambana na Bidhaa Bandia (ACA), bidhaa ghushi vimesheheni zaidi ya asilimia 20 ya soko la mafuta ya petroli.

Kununua lubricants ghushi hakuathiri tu ufanyikazi mzuri wa injini yako, bali pia inakugharimu pesa kwa muda mrefu.

Kampuni ya Vivo Energy Kenya, kampuni inayosambaza na kuuza bidhaa na kutoa huduma za Shell nchini, imezindua jukwaa la kupambana na bidhaa ghushi lililopewa jina la JAZIKA NA SHELL LUBRICANTS.

Wateja watapiga *459* 200# na kuweka kodi iliyo chini ya kifuniko cha mafuta ili kujiandikisha na kushiriki. Wateja pia watapata fursa ya kujipatia na kukusanya pointi ambazo wanaweza kugeuza kuwa zawadi kama vile muda wa maongezi, vocha za ununuzi, tokeni za KPLC na zawadi nyinginezo.

Jukwaa hilo litawawezesha watumiaji kuthibitisha uhalisi wa lubricants za Shell wanazotumia. Kwa njia hii sasa unaweza kuwa na uhakika kwamba unanunua lubricants za Shell zilizo na ubora uliohakikishwa.

Jazika Na Shell Lubricants.