Manufaa ya kukumbatia mfumo mpya wa ETR ulioboreshwa na KRA

Ikiwa unatafuta njia ya kupata mfumo wa ETR, basi kuna aina nne tofauti na ambazo zipo kwa ajili yako!

Muhtasari
  • Kama wewe ni mzalishaji bidhaa, kampuni ya mawasiliano, muuzaji wa jumla au hata msambazaji wa bidhaa, basi mfumo mpya wa ETR unakuhusu sana!
  • Mfumo ulioboreshwa wa ETR una uwezo wa kutathmini kama ankara zako ni sahihi unapofanya mauzo!

Kuwasilisha taarifa ya marejesho ya kodi sasa kumefanywa kuwa rahisi na mfumo mpya wa ELECTRONIC TAX REGISTER (ETR)!

Karibuni,itawezekana kupata taarifa iliyorahisishwa ya marejesho ya kodi! Na hapo itakuwa rahisi na haraka kwako kusanifisha malipo yako ya VAT ili kukuza mazingira mazuri ya kibiashara.

KRA inatia bidii kuhakikisha biashara zote zina nafasi ya kupata manufaa kutokana na mfumo wa ETR ulioboreshwa na pia kuhakikisha marejesho yao ya kodi yanajazwa kwa urahisi kufikia mwisho wa mwaka.

Kama wewe ni mzalishaji bidhaa, kampuni ya mawasiliano, muuzaji wa jumla au hata msambazaji wa bidhaa, basi mfumo mpya wa ETR unakuhusu sana!

Mfumo ulioboreshwa wa ETR una uwezo wa kutathmini kama ankara zako ni sahihi unapofanya mauzo! Utajukumishwa wakati wa kutoa ankara kwa kuwa data hiyo inatumwa na KRA!

Ikiwa unatafuta njia ya kupata mfumo wa ETR, basi kuna aina nne tofauti na ambazo zipo kwa ajili yako!

Aina A – Ni faafu kwa biashara ndogo ambazo utunzaji wa rekodi zao ni wa mwongozo na wale wanaofanya mauzo kwa kuhamahama, k.m. mauzo kwa gari, kwa kuwa mfumo huu wa ETR unaweza kubebeka kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Aina B – Faafu kwa wauzaji wa rejareja na maduka kwa kutumia vituo vya mauzo.

Aina C- Faafu kwa biashara ambazo zinaendesha shughuli zao kiotomatiki na ambazo zinazotumia mifumo ya utozaji ya program za kimitandao/ERPs.

Aina D – Mfumo faafu kwa kila aina ya biashara.

Ni nini kinatokea kwa mfumo wangu wa ETR wa awali ikiwa nitalazimika kuubadilisha?

Pale ambapo mlipa kodi anabadilisha rejista ya kodi aliyokuwa akitumia, anatakiwa kulinda rejista ya kodi iliyotumika awali kulingana na sharti la kuweka kumbukumbu kwa miaka mitano kama ilivyoainishwa katika Kifungu cha 23 cha Sheria ya Taratibu za Ushuru, 2015 (TPA).

Je, mfumo mpya ulioidhinishwa wa ETR una vipengele gani vya ziada?

  1. Uthibitishaji wa data ya ankara katika hatua ya kutoa ankara
  2. Uzalishaji wa msimbo wa kipekee wa QR
  3. Uzalishaji wa nambari ya kipekee ya ankara kwa kila ankara/risiti; nambari ya ankara ya kitengo cha kudhibiti
  4. Uwasilishaji wa ankara ya kodi ya kielektroniki kwa KRA kwa wakati halisi au karibu na wakati halisi
  5. Kukamata PIN ya mnunuzi (hiari); kwa wale tu wanaokusudia kudai VAT kwa malipo ya kuingia
  6. Uzalishaji wa maelezo ya mikopo na madeni ili kurekebisha au kukarabati ankara

Tembelea www.kra.go.ke kwa orodha iliyoidhinishwa ya wasambazaji wa ETR na uboreshe ETR yako leo!