logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanafunzi wa shule ya Maseno afariki baada ya kudondoka kutoka ghorofa la bweni

Mkurugenzi wa Elimu Kanda ya Nyanza Nelson Sifuna alithibitisha kisa hicho, akisema uchunguzi umeanzishwa ili kubaini ni nini kilichosababisha kifo cha kijana huyo.

image
na Davis Ojiambo

Habari26 August 2022 - 12:16

Muhtasari


  • • Mwili wa kijana huyo ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Aga Khan mjini Kisumu.
Shule ya Upili ya Maseno

Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Maseno kaunti ya Kisumu alifariki siku ya Ijumaa baada ya kuanguka kutoka kwa bweni.

Mkurugenzi wa Elimu Kanda ya Nyanza Nelson Sifuna alithibitisha kisa hicho, akisema uchunguzi umeanzishwa ili kubaini ni nini kilichosababisha kifo cha kijana huyo.

Mvulana huyo alianguka kutoka ghorofa ya pili ya bweni katika shule hiyo, Sifuna alisema.

"Tumepokea ripoti kwamba mwanafunzi huyo aliacha barua ya kujiua. Ninataka polisi kuchunguza tuhuma hizo,” aliongeza mkuu huyo wa elimu wa mkoa.

Mwili wa kijana huyo ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Aga Khan mjini Kisumu.

Kwingineko ni kuwa Watu watatu, akiwemo mwanafunzi, walifariki Ijumaa asubuhi, Agosti 26, baada ya lori kugonga basi la shule katika Soko la Ntharene huko Imenti Kusini, Kaunti ya Meru.

Basi hilo lililokuwa likielekea eneo la Kanyakine lilikuwa likisafirisha wanafunzi kuwapeleka shuleni wakati lori lililokuwa likielekea Nkubu lilipoteza mwelekeo na kusababisha ajali hiyo.

Watu watatu, madereva wawili na mwanafunzi walikufa papo hapo. Wanafunzi zaidi ya kumi walijeruhiwa na kupelekwa katika Hospitali ya Misheni ya Consolata, Nkubu.

Miili ya madereva na mwanafunzi huyo ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali hiyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved