Kwa Mungu yote yanawezekana-Ruto asema baada ya uamuzi wa mahakama

Jaji Mkuu Martha Koome alisema Ruto alipata asilimia 50 pamoja na kura moja iliyohitajika ili mmoja atangazwe mshindi.

Muhtasari
  • Katika taarifa yake baada ya Mahakama ya upeo kuidhinisha uchaguzi wake wa urais, Ruto alisema safari yake ya kuwa rais ni ushahidi wa mapenzi ya Mungu
DP RUTO WAKATI WA MANIFESTO YA KENYA KWANZA 30 JUNI 2022
Image: EZEKIEL AMING'A

Rais mteule William Ruto bado amehusisha ushindi wake na Mungu.

Katika taarifa yake baada ya Mahakama ya upeo kuidhinisha uchaguzi wake wa urais, Ruto alisema safari yake ya kuwa rais ni ushahidi wa mapenzi ya Mungu.

"Kwa wanadamu haiwezekani, lakini si kwa Mungu: kwa maana kwa Mungu yote yanawezekana," aliandika.

Mahakama ya upeo ya Kenya Jumatatu ilithibitisha kuchaguliwa kwa William Ruto kama Rais wa tano wa Jamhuri ya Kenya.

Akisoma uamuzi wa Mahakama yaupeo Jumatatu, Jaji Mkuu Martha Koome alisema Ruto alipata asilimia 50 pamoja na kura moja iliyohitajika ili mmoja atangazwe mshindi.

Mnamo Agosti 15, mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alimtangaza Ruto kuwa Rais mteule baada ya kuwashinda Raila na wagombeaji wengine wawili katika uchaguzi wa Agosti 9.

Ruto alipata 7.1m huku Raila Odinga akipata 6.9m kama ilivyotangazwa na IEBC.