EPRA yatangaza kupanda kwa bei ya mafuta

Bei ya petroli imepanda kwa shilingi 20.18 na itauzwa Shilingi 179.30 kwa mwezi mmoja ujao.

Muhtasari

• Bei ya Mafuta ya Taa imeongezeka kwa Sh20 kumaanisha kuwa itauza Sh147.94 jijini Nairobi.

Mhudumu akiweka gari Mafuta ya petroli
Mhudumu akiweka gari Mafuta ya petroli
Image: MAKTABA

Mamlaka ya Udhibiti wa kawi na mafuta nchini imetangaza bei mpya za mafuta.

Katika mabadiliko hayo, lita moja ya mafuta ya petroli imepanda kwa shilingi 20.18 na sasa itauzwa kwa Shilingi 179.30 kwa mwezi mmoja ujao.

Kwa upande mwingine, bei ya dizeli imeongezeka kwa Shilingi 25 na sasa itauzwa shilingi 165 mjini Nairobi.

Bei ya Mafuta ya Taa imeongezeka kwa Sh20 kumaanisha kuwa itauza Sh147.94 jijini Nairobi.

Bei hizo ni pamoja na asilimia 8 ya ushuru wa Ongezeko la Thamani ya bidhaa (VAT).

Kupanda kwa bei ya mafuta kunafuatia kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta kwa bidhaa za petroli na serikali ya Rais William Ruto kama ilivyojulishwa awali.

Ingawa ruzuku ya mafuta ya petroli imeondolewa, ruzuku ya Shilingi 20.82 na 26.25 kwa lita imewekwa kwa dizeli na mafuta ya taa mtawalia.

Mabadiliko ya bei ya mafuta huanza kutekelezwa mara moja.