Rais William Ruto kuondoka nchini kwa ziara rasmi Uingereza na Marekani

Atakuwa miongoni mwa viongozi 500 wa kigeni watakaohudhuria Mazishi ya Malkia Elizabeth II.

Muhtasari

•Rais kwanza ataelekea Uingereza kwanza ambako atahudhuria mazishi ya kitaifa ya Malkia Elizabeth II yaliyopangwa kufanyika Jumatatu.

•Baada ya mazishi, Rais ataondoka kuelekea Marekani ambako atahudhuria Mkutano Mkuu wa 77 wa Umoja wa Mataifa (UNGA) huko New York

Safari ya mwanzo kabisa ya Ruto kama rais
Image: MAKTABA

Rais William Ruto leo ataondoka nchini kwa ziara rasmi nchini Uingereza na Marekani.

Ziara hizo zinakuja takriban wiki moja tu baada yake kuapishwa kama Rais wa tano wa Kenya.

Rais Ruto kwanza ataelekea Uingereza kwanza ambako atahudhuria mazishi ya kitaifa ya Malkia Elizabeth II yaliyopangwa kufanyika Jumatatu.

Mkuu wa nchi anatarajiwa kushiriki chakula cha jioni pamoja  na Mfalme Charles III atakapowasili nchini Uingereza.

Atakuwa miongoni mwa viongozi 500 wa kigeni watakaohudhuria Mazishi ya Serikali ya Malkia Elizabeth II.

Baada ya mazishi, Rais ataondoka kuelekea Marekani ambako atahudhuria Mkutano Mkuu wa 77 wa Umoja wa Mataifa (UNGA) huko mjini New York.

Anatarajiwa kukutana na Rais Joe Biden na maafisa kutoka chumba cha biashara cha Amerika.

Mkutano wa UNGA utakuwa wa kwanza kufanyika ana kwa ana tangu kuanza kwa janga la Covid-19 ambalo lilisitisha kutangamana.

Mikutano ya UNGA mnamo 2020 na 2021 ilifanyikakwa njia ya Kielektroniki.