(+Picha) Rais William Ruto awasili kwenye mazishi ya Malkia kwa basi

Ruto alionekana kuifurahia safari hiyo.

Muhtasari

•Ruto ambaye aliandamana na mke wa rais Rachel alipokelewa na Kamishna Mkuu wa Kenya nchini Uingereza Manoah Esipisu.

•Kiongozi huyo wa nchi aliondoka Kenya Jumapili, kuashiria kuondoka kwake rasmi tangu aapishwe kama Rais Jumanne.

Rais William Ruto aandamana na viongozi wengine kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II
Image: HISANI

Rais William Ruto aliwasili London, Uingereza Jumatatu asubuhi kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II aliyefariki wiki jana.

Ruto ambaye aliandamana na mke wa rais Rachel alipokelewa na Kamishna Mkuu wa Kenya nchini Uingereza Manoah Esipisu.

"Niliwasili London, Uingereza kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II," Ruto alisema katika ujumbe wake wa Twitter Jumatatu.

Baada ya kuwasili, rais pamoja na viongozi wengine walisafirisha kwa basi hadi Westminster Abbey ambako hafla ya mazishi ya malkia inaendelea.

awasili jijini London mnamo Jumatatu asubuhi Septemba 19, 2022
Rais William Ruto awasili jijini London mnamo Jumatatu asubuhi Septemba 19, 2022
Image: TWITTER// WILLIAM RUTO

Ruto ambaye aliungana na mkewe, rais Samia Suluhu wa Tanzania pamoja na viongozi wengine kwenye basi hilo alionekana kuifurahia safari hiyo.

Kiongozi huyo wa nchi aliondoka Kenya Jumapili, kuashiria kuondoka kwake rasmi tangu aapishwe kama Rais Jumanne.

Baada ya mazishi, Ruto ataondoka Uingereza kuelekea Marekani. Ataungana na viongozi wa dunia kwa Kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New