Manufaa ya kuhudhuria hafla ya utalii ya Dubai

Kuna zawadi nyingi ikiwa ni pamoja na safari bila malipo ya kwenda Dubai.

Muhtasari

•Ili kushiriki mchezo, mtu anapaswa kuweka kadi zao za biashara kwenye sanduku na mshindi atachukuliwa kutoka hapo.

•Maonyesho ya barabarani ya DET  yanafanyika nchini Kenya leo, Septemba 22, 2022.

wakati wa hotuba yake katika hoteli ya Movenpick mnamo Septemba 22, 2022
Stella Fubara, mkurugenzi wa Operesheni za Kimataifa Afrika , wakati wa hotuba yake katika hoteli ya Movenpick mnamo Septemba 22, 2022
Image: WILFRED NYANGARESI

Idara ya Uchumi na Utalii ya Dubai (DET) ina mpango mzuri kwa wale ambao watahudhuria Roadshow yao baadae mwezi huu.

Kuna zawadi nyingi ikiwa ni pamoja na safari bila malipo ya kwenda Dubai kwa yeyote atakayeshiriki katika hafla hiyo.

Ili kushiriki katika mchezo wa bahati nasibu wa Dubai, mtu anapaswa kuweka kadi zao za biashara kwenye sanduku na mshindi atachukuliwa kutoka hapo.

Mshindi lazima awepo ili kushinda, kwa hivyo huwezi kuweka kadi yako ya biashara na kumwacha rafiki kuchukua zawadi zako unaposhinda, hata iwe mkeo au mtoto wako.

Dubai inajulikana kwa msukumo wake endelevu wa kuanzisha, kudumisha na kuonyesha mfumo wake salama, wazi na unaoweza kufikiwa.

Hii imeifanya Dubai kuorodheshwa katika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya maeneo bora  ya kitaifa ya kutalii katika Tuzo za Chaguo la Wasafiri la Tripadvisor 2022.

Takwimu mpya za utalii kutoka DET zinaonyesha kuwa kwa ujumla, hoteli za Dubai zilidumisha kiwango cha wastani cha upangaji wa asilimia 76 kuanzia Januari hadi Mei 2022.

Maonyesho ya barabarani ya DET  yanafanyika nchini Kenya leo, Septemba 22, 2022.