Wanafunzi wawili waliotumwa nyumbani wakufa maji wakiogelea mtoni

Mwanafunzi mmoja alizama na kufariki wakati akijaribu kumuoka mwenzake aliyezama.

Muhtasari

•Wawili hao walikuwa pamoja na wenzao wengine wawili kutoka taasisi moja wakati kisa hicho kilipotokea.

•Wanafunzi hao walipita katika kanisani ili kuona uongozi wa kanisa kabla ya tukio hilo la bahati mbaya kutokea.

Wakazi wakizunguka gari la polisi lililokuwa limebeba mwili wa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Sibuoche uliotolewa kutoka mto Migori.
Wakazi wakizunguka gari la polisi lililokuwa limebeba mwili wa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Sibuoche uliotolewa kutoka mto Migori.
Image: MANUEL ODENY

Wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari ya Sibuoche walikufa maji katika mto Migori siku ya Ijumaa baada ya kuondoka shuleni kuelekea nyumbani.

Wawili hao walikuwa pamoja na wenzao wengine wawili kutoka taasisi moja wakati kisa hicho kilipotokea.

Watazamajiiawalisema wanafunzi hao walipita katika kanisa la Church of God of Prophecy lililopo katika maeneo ya Jua kail,mjini Migori kuona uongozi wa kanisa kabla ya tukio hilo la bahati mbaya kutokea.

Mchungaji wa kanisa hilo Joshua Kangie alisema wanafunzi hao huwa wanapita kanisani hapo kabla ya kuondoka kuelekea makwao.

"Walipokuwa wakisubiri viongozi wa kanisa, wanne hao waliamua kuogelea katika mto wa karibu wa Migori tukio la bahati mbaya lilipotokea, bado tuna mshtuko," Kangie alisema.

Watazamaji walisema wanafunzi hao walikuwa wakifurahia kuogelea mtoni wakati mmoja wao alipoanza kuzama baada ya kuelea kwenye kina kirefu cha mto huo.

Mwenzake akaingia mbio kumuokoa na wote wawili wakazama.

"Wengine wawili walikimbia na kuwaita mafundi wa jua kali na kikundi cha watu waliokuwa wakiosha magari karibu ambao walifika, lakini walikuwa wamechelewa," Jane Akinyi, mfanyabiashara alisema.

Juhudi za kutafuta miili zilianza mara moja na mwili mmoja ulitolewa huku mwingine ukiendelea kutafutwa hadi wakati wa kwenda kwa waandishi wa habari.

Wakaazi walisema tukio hilo ni la kusikitisha na kuitaka idara ya zimamoto ya serikali ya kaunti ya Migori kuajiri wapiga mbizi ili kusaidia katika utafutaji na uchukuaji wa maiti.

“Tumefaulu kuuchukua mwili huo baada ya wafanyakazi wa kujitolea na wanachama wa Msalaba Mwekundu wa Kenya kuja kusaidia. Tunatoa changamoto kwa idara ya zimamoto ya kaunti kutusaidia wakati ujao na wapiga mbizi,” Albert Opiyo, mzamiaji alisema.