Rais Ruto atuma rambirambi kwa watu wa Tanzania kufuatia ajali ya ndege

Precision Air ndiyo shirika kubwa la ndege la kibinafsi la Tanzania na kwa kiasi fulani inamilikiwa na Kenya Airways.

Muhtasari
  • Ndege hiyo yenye ilianguka katika Ziwa Victoria Jumapili asubuhi ilipokuwa ikijaribu kutua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba
Rais wa tano wa Kenya
WILLIAM RUTO Rais wa tano wa Kenya
Image: Facebook//WILLIAMRUTO

Rais William Ruto ametuma ujumbe wa rambirambi kwa watu wa Tanzania kufuatia ajali mbaya ya ndege iliyogharimu maisha ya watu 19.

Ndege hiyo yenye ilianguka katika Ziwa Victoria Jumapili asubuhi ilipokuwa ikijaribu kutua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba.

"Kenya inaomboleza pamoja na watu wa Tanzania kufuatia ajali mbaya ya ndege. Tunatuma rambirambi zetu na tunawatakia afueni ya haraka manusura wote wa mkasa huo wa Precision Air," Ruto alisema.

Orodha ya waathiriwa iliyotolewa na mamlaka ya Tanzania ilionyesha kuwa Wakenya wawili walikuwa ndani ya ndege ya Precision Air.

Ndege hiyo ilikuwa ikitoka Dar es Salaam kuelekea Bukoba kupitia Mwanza.

Precision Air ndiyo shirika kubwa la ndege la kibinafsi la Tanzania na kwa kiasi fulani inamilikiwa na Kenya Airways. Ilianzishwa mnamo 1993 na inaendesha safari za ndege za ndani na kikanda.