Ruto:Kwa miaka 5 tumerudisha chini asimilia ya viwanda

Rais aliahidi kuanzisha mfumo unaokuza sekta ya viwanda, kutengeneza ajira kwa wananchi na kuokoa fedha za kigeni.

Muhtasari
  • "Katika miaka 5 iliyopita, walaghai wa kati, madalali wamehakikisha kuwa sera ya serikali inapotoshwa na kupendelea bidhaa zinazoagizwa kutoka nje
RAIS WILLIAM RUTO
Image: PCS

Rais William Ruto amedai kuwa ukuaji wa viwanda nchini Kenya ulishuka katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kutokana na madai ya hujuma kutoka kwa watu wachache aliowataja kama "walaghai na madalali."

Akiongea alipoagiza viwanda vya kutengeneza chuma vya Devki katika Kaunti ya Kwale, Rais aliapa kubadilisha maovu haya na kuboresha mchango wa ukuzaji wa viwanda katika Pato la Taifa kuendelea.

Rais aliahidi kuanzisha mfumo unaokuza sekta ya viwanda, kutengeneza ajira kwa wananchi  na kuokoa fedha za kigeni.

“Kwa miaka miaka, tumerudisha chini percentage ya industrialization kutoka 9% mpaka 7% ya GDP….na ni kwa sababu ya sera ambayo haifai. Watu wachache wanafanya urafiki na mabadiliko ya serikali, wanapindua sera ili kusaidia brokers, middlemen kuhangaisha viwanda vyetu. Nataka niwahakikishie kwamba tutabadilisha mtindo huo," alisema.

"Katika miaka 5 iliyopita, walaghai wa kati, madalali wamehakikisha kuwa sera ya serikali inapotoshwa na kupendelea bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, kwa sababu wanapata pesa kidogo, na wametatiza ukuaji wa viwanda nchini Kenya. Kampuni kumi na sita za kusaga chuma nchini Kenya zimefungwa kwa sababu madalali wamebadilisha sera ili kupendelea bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.”