Mwanamume ajisalimisha kwa polisi baada ya kumuua mwanamke,adai aligeuka jini

Kisha akawaambia polisi kwamba alimdunga kisu mwanamke huyo mara nyingi mgongoni na kichwani

Muhtasari
  • “Anadai walikutana kwenye baa kabla haijachanua kuwa kitu tofauti. Kisha hili likatokea,” alisema
Crime scene
Crime scene

Mwanamume mwenye umri wa miaka 59 amejisalimisha kwa polisi huko Kasarani baada ya kudaiwa kumuua mwanamke aliyekutana naye katika baa moja huko Zimmerman.

Polisi walisema mshukiwa, Wangethi Chege, alifika katika kituo cha polisi Jumanne na kuwataka maafisa katika ofisi ya ripoti kwenda kuchukua mwili wa marehemu.

Mkuu wa polisi wa Kasarani Anthony Mbogo alisema maafisa wake walipoenda kwenye nyumba hiyo, walipata mwili huo.

Alisema mtuhumiwa huyo alisema alikutana na marehemu katika kituo cha burudani cha mtaani kisha kumpeleka nyumbani kwake.

“Anadai walikutana kwenye baa kabla haijachanua kuwa kitu tofauti. Kisha hili likatokea,” alisema.

Kisha akawaambia polisi kwamba alimdunga kisu mwanamke huyo mara nyingi mgongoni na kichwani, akidai alikuwa amegeuka jini.

"Alisema aliogopa kwamba angeweza kumdhuru. Kwa hivyo, aliamua kumuua,” bosi wa polisi alisema.

Polisi walimzuilia baada ya kushughulikia eneo la tukio.

Wanapanga kumfikisha mshukiwa mahakamani kuomba siku zaidi wanapochunguza tukio hilo. Mbogo alisema pamoja na mengine, watapima utimamu wake wa kiakili.

Alisema walipata visu viwili vinavyosadikiwa kutumika kutekeleza uhalifu huo.