Polisi wamsaka mshukiwa aliyemlawiti mwanamume mlevi Bomet

Polisi wametoa wito kwa wananchi kuripoti taarifa zozote zitakazosaidia kumkamata.

Muhtasari
  • Mwathiriwa aliokolewa na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Longisa kwa matibabu
crime scene
crime scene

Polisi wanamsaka mshukiwa aliyemlawiti mwanamume mlevi huko Bomet.

Katika taarifa yake siku ya Jumatano, Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ilisema kwamba mwathiriwa alifungiwa ndani ya nyumba ya washukiwa kwa zaidi ya saa 10.

DCI alisema kuwa mwanamume huyo alipokuwa akirejea kwenye baa hiyo, mshukiwa alimwendea na kumpeleka hadi nyumbani kwake umbali wa takriban mita 200.

DCI ilisema juhudi za mwanamume huyo kuzua taharuki hazikufaulu kwa sababu ya sauti kubwa ya muziki kutoka kwa baa hiyo.

Polisi waliongeza kuwa mshukiwa alimlawiti mwathiriwa asiyejiweza mwenye umri wa miaka 33 hadi Jumanne alasiri wakati mpita njia alipomuokoa.

Mwathiriwa aliokolewa na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Longisa kwa matibabu.

Polisi wameanzisha msako wa kumsaka mshukiwa aliyetoroka nyumbani kwake.

Polisi wametoa wito kwa wananchi kuripoti taarifa zozote zitakazosaidia kumkamata.