Mkenya aibuka shujaa Qatar baada ya video akiwaelekeza wageni kusambaa

Mwanamume huyo alikuwa amepata kazi ya ulinzi huko Qatar .

Muhtasari

• Abubakr Abbass ni Mkenya mzaliwa wa Mombasa.

• Alituzwa kwa kujitolea na bidii yake ya kuwasaidia watu kujua njia ya kwenda kwenye uwanja wa kombe la dunia.

Mwanamume mmoja Mkenya ameshabikiwa mitandaoni na kujulikana kote duniani baada ya video yake kusamba alipokuwa akitumia kipaza sauti akiwaelekeza mashabiki kwenye njia ya kwenda Doha Qatar kulikokuwa kumeandaliwa michuano ya kombe la dunia.

Abubakr Abbass mwenye umri wa miaka 23 na aliyezaliwa Mombasa amekuwa mtu wa kipekee na kipenzi cha wengi kwenye mitandao ya kijamii kutokana na ubunifu na tajriba alionayo ya kuwachekesha watu waliokuwa wamekuja kujionea michezo ya Kombe la Dunia inayoendelea Qatar.

Kwenye video hiyo iliyopakiwa kweye mitandao yote ya kijamii Abbass alionkana amekaa kwenye kiti. Mkono wa kushoto alikishika kipaza sauti huku mkono wake wa kulia amevalia chombo chenye ishara kubwa ya kuwaelekeza watu. Alisema kuwa  ''Qatar! Pita njia hii'' huku akirudia rudia maneno hayo yaliowachekesha sio tu waliokuwa karibu pia walioitazama video hiyo.

Watu mbali mbali wa nchi zingine kama vile Uchina wanaonekana kumuiga Abbass huku wakikosa kuficha kicheko chao.

Abbass alipata kazi kama mlinzi ndani ya uwanja wa Kombe la Dunia na  jukumu lake lilikuwa kuwaelekeza watu wasiojua Doha jiji kuu la Qatar.

Alisema kuwa safari yake ya kupata kazi hiyo haikuwa rahisi vile kwani nusura akose ila anajivunia mchango anao utoa kwenye michuano hio ya  Kombe la Dunia la 2022.

"Yaani naeza sema ni  Mungu tu. Kwani siku ya kuchukuliwa kazi nilienda siku ya mwisho wakati shughuli hiyo ilikuwa ikikamilika. Kwa bahati njema  nikapigiwa simu  na ujumbe mfupi baadaye nikaambiwa nimefaulu interview. Nirirukaruka na kumwomba Mungu kwani alikuwa amenipangia mema.'' Alieleza Abbass kwenye video nyingine.

Kijana huyo anazidi kutuzwa  kwa  ubunifu wake wa kufanya kazi yake kwa bidii na kujitolea kwa udi na ambari.

Abubakar Abbas akiwaelekeza mashabiki wa kombe la dunia njia.
Abubakar Abbas akiwaelekeza mashabiki wa kombe la dunia njia.
Image: Facebook
Abubakar Abbas akiwaelekeza mashabiki wa kombe la dunia njia.
Abubakar Abbas akiwaelekeza mashabiki wa kombe la dunia njia.
Image: Facebook
Abubakar Abbas akiwaelekeza mashabiki wa kombe la dunia njia.
Abubakar Abbas akiwaelekeza mashabiki wa kombe la dunia njia.
Image: Facebook