Linturi ajitenga na matamshi ya Kuria kuhusu uingizaji wa mahindi kutoka nje ya nchi

Linturi amesema yeye ndiye mlinzi wa kiasi gani cha chakula tunachohitaji na upungufu ni kiasi gani.

Muhtasari
  • “Kwa hiyo sitajibu kinachoripotiwa kwenye mitandao ya kijamii,” alisema.
  • "Shika farasi wako maana nataka kukupa msimamo ambao niko tayari kuutetea. Nahitaji kuwa na takwimu kabla sijajibu hilo."
WAZIRI WA KILIMIO MITHIKA LINTURI
Image: CHARLENE MALWA

Waziri wa Kilimo Mithika Linturi amejitenga na maoni ya Waziri wa Biashara Moses Kuria kuhusu uingizaji wa mahindi.

Linturi amesema yeye ndiye mlinzi wa kiasi gani cha chakula tunachohitaji na upungufu ni kiasi gani.

“Kwa hiyo sitajibu kinachoripotiwa kwenye mitandao ya kijamii,” alisema.

"Shika farasi wako maana nataka kukupa msimamo ambao niko tayari kuutetea. Nahitaji kuwa na takwimu kabla sijajibu hilo."

Linturi alisema kwammba atatoa ripoti ya kina kuhusu chakula, atakapokuwa na data kamili.

"Nitatoa ripoti ya kina zaidi kuhusu hali ya chakula kitaifa baadaye nikiwa na data yote. Tulia, utakuwa na chakula," Linturi alisema.

Waziri Kuria amekuwa akikosolewa  vikali mitandaoni baada ya matamshi yake ya uingizaji mahindi.

Jumamosi Kuria aliwapa wakulima saa 72 ili kutoa mahindi yaliyokuwa yamehifadhiwa la si vyo mahindi kutoka nje ya nchi yaingizwe.