Msiba! Wanawake watatu wapigwa na radi hadi kufa Vihiga

Wanawake hao walikuwa wamejificha chini ya kibanda kando ya barabara.

Muhtasari

•Watu kadhaa waliofika eneo la tukio walisema wawili kati yao ni wauza ndizi katika mji wa Luanda na wa tatu ni msichana mwenye umri wa makamo.

•OCPD wa eneo la Luanda, David Ndirangu alithibitisha kisa hicho

Crime Scene
Image: HISANI

Wanawake watatu kutoka mji wa Luanda, kaunti ya Vihiga walipigwa na radi hadi kufa wakati wa mvua kubwa siku ya Jumapili jioni.

Wanawake hao walikuwa wamejificha chini ya kibanda kando ya barabara.

Bado ha

Hata hivyo, watu kadhaa waliofika eneo la tukio walisema wawili kati yao ni wauza ndizi katika mji wa Luanda na wa tatu ni msichana mwenye umri wa makamo.

OCPD wa eneo la Luanda, David Ndirangu alithibitisha kisa hicho na kusema alifahamishwa kuhusu suala hilo.

"Nimefahamishwa na mamlaka ya eneo hilo kwamba watu watatu wameuawa na radi wakati wa mvua ya jioni hii," Ndirangu alisema Jumapili jioni.

"Ni bahati mbaya kwamba wanawake hao watatu walikuwa wamechukua kivuli kwenye kioski kando ya barabara," aliongeza.

Miili yao ilikuwa imelala kando ya barabara nyuma ya Hoteli ya Triple T katika kaunti ndogo ya Luanda kabla ya kuchukuliwa na maafisa.