Mfanyabiashara Francis Kiambi alikufa kutokana na mshtuko wa Moyo -Upasuaji

Haya yalifichuliwa Ijumaa kufuatia uchunguzi wa mwili wake uliofanywa na Mwanapatholojia Mkuu wa Serikali Johansen Oduor.

Muhtasari
  • Mwili wa marehemu ulihamishwa hadi nyumbani makafani ya Lee Funeral baada ya daktari wa familia kutoka hospitali ya karibu ya Karen kuthibitisha kifo hicho
FRANCIS KIAMBI
Image: KWA HISANI

Marehemu mfanyabiashara Francis Kiambi ambaye alipatikana amefariki nyumbani kwake Karen, Nairobi mnamo Jumatatu, Januari 9 alifariki kutokana na mshtuko wa moyo.

Haya yalifichuliwa Ijumaa kufuatia uchunguzi wa mwili wake uliofanywa na Mwanapatholojia Mkuu wa Serikali Johansen Oduor.

Kulingana na Dkt Oduor, mshtuko wa moyo ulisababishwa na ugonjwa wa Coronary Artery kutokana na mafuta nyingi katika mwili wa marehemu.

Katika mshtuko wa moyo, kifo kinaweza kutokea haraka ikiwa hatua hazitachukuliwa mara moja.

Ripoti ya polisi ilionyesha kwamba kifo cha Bw. Kiambi kiliripotiwa na mkewe Mary Waigwe Muthoni ambaye aliwaambia polisi kwamba walirudi nyumbani pamoja na mumewe mwendo wa saa sita usiku Jumapili baada ya kukaa. wakati fulani kwenye jumba la burudani huko Karen.

Inasemekana kuwa wanandoa hao waliingia kwenye ugomvi wa kinyumbani baada ya mkewe kudaiwa kukataa kuwa mdhamini wa mumewe katika kupata mkopo wa Ksh.2 bilioni aliokuwa akitafuta kufungua biashara.

Baada ya kutofautiana, inasemekana wawili hao walikwenda kulala katika vyumba tofauti, lakini mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 50,alipatikana amekufa na matapishi kando ya kitanda chake.

Mwili wa marehemu ulihamishwa hadi nyumbani makafani ya Lee Funeral baada ya daktari wa familia kutoka hospitali ya karibu ya Karen kuthibitisha kifo hicho.