Mshukiwa wa mauaji ya kinyama ya msomi Gerishon Mwiti aliyeuawa kinyama Nairobi akamatwa

Operesheni hiyo iliendeshwa na kikosi cha maafisa kutoka Ofisi ya Utafiti wa Uhalifu na Ujasusi yenye makao yake makuu katika kaunti ya Nairobi,

Muhtasari
  • Kulingana na DCI Mshukiwa Bernard Kioko, ambaye alikuwa mtunza bustani katika nyumba ya Dkt. Mwiti amekamatwa muda mfupi uliopita Mabatini katika makazi ya Mathare
Mshukiwa wa mauaji ya mashauri wa jiji aliyeuawa Jumamosi ametiwa mbaroni
Image: DCI/TWITTER

Mshukiwa mkuu wa mauaji ya kinyama ya msomi na mwanzilishi wa taasisi ya uongozi nchini mwenye umri wa miaka 81 Dkt Gerishon Mwiti, ambaye aliuawa kwa kukatwakatwa mnamo Januari 14, 2023 katika mtaa wa Thigiri huko Westlands kaunti ya Nairobi, amekamatwa.

Kulingana na DCI Mshukiwa Bernard Kioko, ambaye alikuwa mtunza bustani katika boma la marehemu alikamatwa siku ya Jumatano eneo la Mabatini katika mtaa wa Mathare, baada ya kuwa mafichoni tangu kufanyika kwa tukio hilo Jumamosi iliyopita.

"Kulingana na mtoto wa marehemu Daniel Mwiti, alipata mwili usio na uhai  kwenye bustani yao ukiwa na  alama ya kukatwa sehemu ya nyuma ya kichwa chake,"Idara ya DCI ilisema.

DCI ilisema oparesheni ya kumsaka ilichukua zaidi ya saa 24, huku mshukiwa akiwachezea maafisa wa polisi mchezo wa paka na panya akijificha Mwingi kaunti ya Kitui na kuhamia maeneo ya Mathare alikokamatwa.

Msako huo uliendeshwa na kikosi cha maafisa wa vitengo mbali mbali vya polisi.