Nyamu apewa muda zaidi na kamati ya nidhamu ya UDA kujibu mashtaka dhidi yake

Alifika mbele ya kamati hiyo siku ya Ijumaa ambapo kikao hicho kiliahirishwa hadi Februari 24 saa tatu asubuhi.

Muhtasari
  • Baadhi ya Wakenya walitaka afukuzwe katika chama na kusema kuwa amekiuka Sura ya Sita ya Katiba kuhusu Uongozi na Uadilifu
Nyamu asema haachi pombe
Nyamu asema haachi pombe
Image: Facebook

Seneta mteule Karen Nyamu amepewa muda zaidi na kamati ya nidhamu ya UDA kujibu tuhuma dhidi yake.

Alifika mbele ya kamati hiyo siku ya Ijumaa ambapo kikao hicho kiliahirishwa hadi Februari 24 saa tatu asubuhi.

"Seneta aliruhusiwa muda zaidi kujibu tuhuma zilizotolewa dhidi yake na mwanachama wa chama," chama cha United Democratic kilisema kwenye notisi.

Mashtaka dhidi ya seneta yanahusu mwenendo wake 'wa aibu' mnamo Desemba 16, 2022

Mbunge huyo alizua taharuki katika tamasha la msanii wa Mugithi Samidoh mjini Dubai na kusababisha mzozo na mkewe Edday Nderitu.

Katika kipande cha video ambacho kilisambaa mtandaoni, Nyamu alionekana akizuiliwa na walinzi wa tukio hilo wakati wa tamasha hilo.

Klipu tofauti ilionyesha Nyamu akicheza dansi jukwaani huku mwimbaji Samidoh na Karangu Muraya wakitumbuiza washereheshaji muda mfupi kabla ya kuondolewa baada ya ugomvi.

Seneta huyo baadaye alilaumu pombe kwa ajili ya matendo yake , tabia ambayo aliapa kuacha Januari mwaka huu.

Baadhi ya Wakenya walitaka afukuzwe katika chama na kusema kuwa amekiuka Sura ya Sita ya Katiba kuhusu Uongozi na Uadilifu.

Aliyekuwa mgombea urais wa UDA Japhnei Orina alikuwa miongoni mwa waliotoa wito kwa chama hicho kuanza mchakato wa kumtimua.