DP Gachagua afichua kazi ya Dennis Itumbi katika ikulu

Gachagua alifichua kuwa Itumbi ni msaidizi wa karibu wa Rais William Ruto.

Muhtasari

•“Wengi mnajiuliza ni kazi gani ya Itumbi. Ofisi yake ni, kuja hapa nenda huko. Ni rafiki wa karibu wa Rais wetu,” alisema.

• Gachagua aliambia waumini kuwa wanapaswa kumshukuru Mungu kwa kuwa Itumbi yuko hai.

Naibu rais Rigathi Gachagua
Image: MAKTABA

Naibu Rais Rigathi Gachagua amefichua kazi ambayo Dennis Itumbi  huwa anafanya katika Ikulu.

Akizungumza mjini Kerugoya siku ya Jumapili, Gachagua alifichua kuwa Itumbi ni msaidizi wa karibu wa Rais William Ruto.

“Wengi mnajiuliza ni kazi gani ya Itumbi. Ofisi yake ni, kuja hapa nenda huko. Ni rafiki wa karibu wa Rais wetu,” alisema.

Gachagua alikuwa akijibu wakosoaji kutoka upande wa Azimio waliodai kuwa Itumbi alitengwa na Ruto alipokuwa akiunda timu yake ya mawasiliano Ikulu.

Mwanablogu Dennis Itumbi aliruhusiwa kutoka hospitalini
Mwanablogu Dennis Itumbi aliruhusiwa kutoka hospitalini
Image: HANDOUT

"Itumbi hana afisa bali ndiye anayesimamia kila kitu. Anapanga kila kitu," alisema

Aidha Gachagua aliambia waumini kuwa wanapaswa kumshukuru Mungu kwa kuwa Itumbi yuko hai.

Alidai kuwa Itumbi alikaribia kuuawa lakini ni kwa neema ya Mungu alinusurika.

DP pia alishukuru umma kwa kuwa 'wafichuzi' wakati Itumbi ilipotekwa nyara.

Licha ya Gachagua kukiri kuwa biblia inasema tuwasamehe wakosaji, alisema baadhi ya visa ni vigumu kusamehe na kusahau.

"Askofu wetu amehubiri kuhusu msamaha lakini baadhi ya matukio ni magumu kusahau," alisema.

Mwezi Desemba 2020, Itumbi alisema anatekeleza jukumu muhimu katika utawala wa Ruto.

"Nina jukumu muhimu sana ambalo ni, njoo hapa, nenda pale. Hilo ni jukumu muhimu sana katika serikali," alisema.

Alipotakiwa kufafanua uvumi ulioenea kuwa anateuliwa kuwa Msemaji wa Serikali, Itumbi alisema hayo ni matamanio makubwa lakini msimamo wake kwa sasa ni ‘njoo huku, nenda kule’.

Utafsiri: Samuel Maina