Tukutane Kamukunji-Raila asema baada ya kurejea nchini

Odinga alipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), na wakuu wa Azimio, akiwemo Martha Karua na Kalonzo Musyoka.

Muhtasari
  • Waziri Mkuu huyo wa zamani alikuwa ametangaza kwamba atafanya mazungumzo ya umma katika uwanja wa Kamukunji, Nairobi, muda mfupi baada ya kutua nchini
Image: RAILA ODINGA/TWITTER

Kiongozi wa Chama cha Azimio alirejea Nchini Jumatatu, Januari 23, kutoka kwa safari ya kikazi nchini Afrika Kusini.

Odinga alipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), na wakuu wa Azimio, akiwemo Martha Karua na Kalonzo Musyoka.

Wengine katika uwanja huo wa ndege ni aliyekuwa Katibu wa Baraza la Mawaziri Eugene Wamalwa, msemaji wa Chama cha Azimio Makau Mutua,Jeremiah Kioni,Wycliffe Oparanya miongoni mwa viongozi wengine.

Nimefurahi kurejea nyumbani, tukutane Kamukunji," Raila alisema.

Waziri Mkuu huyo wa zamani alikuwa ametangaza kwamba atafanya mazungumzo ya umma katika uwanja wa Kamukunji, Nairobi, muda mfupi baada ya kutua nchini.

Mkutano huo ulipangwa baada ya mdokezi kudai kwamba alikuwa na ushahidi wa wizi mkubwa uliotokea katika Mlima Kenya wakati wa  uchaguzi mkuu wa Agosti 9.