Raila Odinga atuma risala za rambirambi kwa familia ya Magoha

Raila amesema kwamba Profesa huyo atakumbukwa kwa mchango wake katika sekta ya elimu.

Muhtasari
  • Magoha aliaga siku ya JUmanne, katika hspitali ya Nairobi alipokuwa akipokea matibabu
CS magoha
CS magoha
Image: Picha:Hisani

Kinara wa muungano wa Azimio Raila Odinga ametuma risala za Rambirambi kwa aliyekuwa waziri wa elimu George Magoha.

Raila amesema kwamba Profesa huyo atakumbukwa kwa mchango wake katika sekta ya elimu.

"Nimesikitishwa sana na kifo cha Prof. George Magoha, kiongozi wa mabadiliko, msomi mashuhuri, mtumishi wa umma aliyejitolea, na daktari mashuhuri ambaye aliacha alama isiyofutika katika mfumo wa elimu wa nchi yetu...."

Aliendelea;

"Tutamkumbuka kwa mchango wake. akili ya ajabu, akili na uwezo wa kututia moyo na kutoa changamoto ya kufanya tuwezavyo

Rambirambi zangu ziende kwa familia yake na wafanyakazi wenzake. Apumzike kwa Amani ya Milele."

Magoha aliaga siku ya JUmanne, katika hspitali ya Nairobi alipokuwa akipokea matibabu.

Huku wakitangaza kifo chake walisema;

"Ni kwa masikitiko makubwa kwamba tunatangaza kifo cha ghafla na kisichotarajiwa cha Profesa George Magoha jioni hii katika Hospitali ya Nairobi," Mkurugenzi Mtendaji wa The Nairobi Hospital James Nyamongo alisema katika taarifa.