Polisi waomba siku 7 kuwazuilia walimu waliokamatwa kufuatia video chafu, Kisii

Wanahitaji kuwazuilia walimu hao kwa siku saba zaidi ili kukamilisha uchunguzi kuhusu kisa hicho cha kutamausha.

Muhtasari

• Katika video hiyo, wavulana hao waliovalia sare za shule wanalazimishwa na walimu wao kufanya kitendo kichafu huku wakiwa wamelala juu ya kila mmoja nao wao wakiwatazama kwa kicheko.

Picha: KWA HISANI
Picha: KWA HISANI

Polisi katika Kaunti ya Kisii wanatafuta kuwazuilia walimu saba waliokamatwa Jumatano kufuatia video iliyosambaa mtandaoni iliyonasa wanafunzi wakifanyiwa kitendo kichafu kilichotokea katika Shule ya Msingi ya Itumbe DOK huko Nyamache.

Katika video hiyo, wavulana hao waliovalia sare za shule wanalazimishwa na walimu wao kufanya kitendo kichafu huku wakiwa wamelala juu ya kila mmoja nao wao wakiwatazama kwa kicheko.

Akizungumza siku ya Alhamisi, OCPD wa Nyamache Kipkulei Kipkemboi alisema wanahitaji kuwazuilia walimu hao kwa siku saba zaidi ili kukamilisha uchunguzi kuhusu kisa hicho cha kutamausha.

“Tulifanikiwa kuwawasilisha mbele ya mahakama kwa madhumuni ya kuomba siku 7 zaidi kuwazuilia huku tukiendelea kufanya uchunguzi,” alisema Kipkemoi.

Kulingana na afisa huyo wa polisi, walimu sita walikamatwa kisha wa saba alinaswa baada ya kuhojiwa zaidi.

Sita hao walikuwa Everline Moraa, Gladys Kenyanya, Angelina Joseph, Moraa Nyairo, Cathrine Mokaya na William Isoka. Walikamatwa baada ya maafisa wa Wizara ya Elimu katika kaunti hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kaunti Ndogo ya Nyamache Linet Onduso kuzuru shule hiyo baada ya kupokea video hiyo.