Waalimu walioonekana katika video ya watoto wakiigiza ngono kukabiliwa na hatua za kinidhamu

Muhtasari

• Katika video hiyo, watu wazima wanaoshukiwa kuwa walimu wanasikika wakijadiliana na kucheka kwa sauti huku mtu

WAZIRI WA ELIMU EZEKIEL MACHOGU
Image: ANDREW KASUKU

Waalimu sita kutoka shule ya msingi ya Itumbe DOK nchini Kenya wanaoshutumiwa kwa kuwalazimisha watoto kuigiza ngono wanakabiliwa na hatua ya nidhamu na kufutwa kazi, amesema Alhamisi Waziri wa elimu Ezekiel Machogu.

Awali waalimu hao wa shule ya msingi walikamatwa na polisi kufuatia kanda ya video iliyoshirikishwa mitandaoni ikiwaonyesha wanafunzi wakiiga kitendo cha ngono huku waalimu wakiwatazama.

Taarifa za vyombo vya habari nchini humo zinaripoti kuwa walimu hao wa Nyamache, katika jinbo la Kisii, walikamatwa baada ya maafisa wa wizara ya elimu kutazama video hiyo na kutoa malalamiko.

Katika video hiyo, watu wazima wanaoshukiwa kuwa walimu wanasikika wakijadiliana na kucheka kwa sauti huku mtu akiwarekodi wavulana wanne ambao wamevalia sare za shule.

Ripoti ya polisi ilibainisha kuwa klipu "kuwafichua wanafunzi katika kitendo kichafu" ilionekana kuwa ilitoka shuleni. Ilisema sita waliokamatwa walikuwa wakisaidia katika uchunguzi na mashtaka yanayofaa yatafuata.

Video hiyo ilizua taharuki kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakitaka hatua zichukuliwe.

"Walichofanya kinaweza tu kuitwa tukio la kishenzi, kinyama, na kichaa. Haina uhalali wowote! Wacha wakabiliane vikali kisheria,”

Mkenya mmoja kwenye Twitter alisema. "Naunga mkono kukamatwa kwa walimu hao sita ... Hakuna uhalali [wa] walichokifanya,"