Wabunge waunga mkono hoja dhidi ya mashoga, wasagaji

Wabunge wengi walisema ushoga ni vitendo vya kutisha ambavyo havipaswi kuruhusiwa katika jamii,

Muhtasari

• Mbunge wa Nyali Mohamed Ali amewasilisha hoja inayolenga kuzuia mjadala wa umma kuhusu wasagaji, mashoga, watu wa jinsia mbili, waliobadili jinsia, na watu wengine wenye hulka zisizo za kawaida za mapenzi.

Wabunge wakiwa katika ukumbi wa bunge wa mijadala
MAKTABA Wabunge wakiwa katika ukumbi wa bunge wa mijadala

Bunge sasa linataka wanaounga mkono na wale katika uhusiano wa jinsia moja kuadhibiwa vikali.

Wabunge siku ya Jumatano waliunga mkono hoja ya Mbunge wa Nyali Mohamed Ali ambayo inalenga kuzuia mjadala wa umma kuhusu wasagaji, mashoga, watu wa jinsia mbili, waliobadili jinsia, na wengine wenye hulka zisizo za kawaida.

Wakichangia wakati wa mjadala huo, wabunge walitaka sheria kali zitakazohakikisha kwamba wale wanaoeneza na kutekeleza LGBTQ wanaadhibiwa.

Naibu Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa na Mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya alitoa wito wa kuwepo kwa sheria itakayotoa adhabu kali zaidi. Mbunge huyo hata hivyo alionya dhidi ya sheria hiyo akisema kuwa jambo hilo linashughulikiwa kikamilifu kwa katiba  katiba ya Kenya.

"Ingekuwa bora kama mheshimiwa mbunge angependekeza mabadiliko ya Kanuni ya Adhabu ili kuweka adhabu kali kwa wale wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kwa vile suala hili tayari limekatazwa," alisema.

Ali amependekeza kupiga marufuku kuzungumza, kuchapisha na kusambaza habari kuhusu LGBTQIA.

Akinukuu Kifungu cha 33 cha Katiba, Baya alibainisha wakati ushoga ni kinyume na maadili ya familia yaliyowekwa kisheria, alisema katiba tayari imeharamisha uhusiano wa jinsia moja.

"Tusijihusishe na zoezi ambalo tayari limeshatolewa kwenye sheria, katiba tayari imeharamisha kwamba, hatuwezi kuja hapa kwa lengo la kupunguza uhuru wa kujieleza," alisema.

Lakini Mbunge wa Nakuru Mashariki David Gikaria alisema hoja mbele ya Bunge inalenga kuwaadhibu wale ambao watakuwa wakieneza maadili ya LGBTQIA katika jamii.

"Hoja hiyo inahusu kutoa hukumu kali kwa wale wanaofanya uhusiano wa jinsia moja," Gikaria alisema kwa utaratibu.

Mbunge wa Kitui Kusini Rachel Nyamai aliunga mkono hoja hiyo akisema adhabu kali zinafaa kuwekwa kwa wale wanaosambaza habari zinazounga mkono LGBTQIA na wale wanaofanya hivyo.

"Hivi ni vitendo vya kutisha ambavyo havipaswi kuruhusiwa katika jamii," alisema akilaumu uamuzi wa Mahakama ya Juu kuhusu utambuzi wa haki za LGBTQIA.

"Wanaofanya mambo haya wanaanza kujutia matendo yao, mjadala unazidi kupamba moto vijiweni na wanajadili suala hili kwa sababu linazungumzwa sana...tuseme hapana."

Mbunge wa Luanda alilaani uenezaji wa habari kuhusu LGBTQIA akisema kama vile Mungu alivyoharibu Sodoma na Gomora katika Biblia kuhusu ukosefu wa maadili, serikali haipaswi kuruhusu hali hiyo nchini.

"Tuseme hapana kwa LGBTQIA katika nchi hii ambayo inamcha Mungu, mjadala huu haupaswi kuruhusiwa miongoni mwa wakazi wa nchi," alisema. 

Mbunge wa Malindi Amina Laura aliunga mkono hoja hiyo akisema maadili, tamaduni na itikadi  za nchi hazizingatii uhusiano wa jinsia moja. 

TAFSIRI : DAVIS OJIAMBO.